In Summary

• Takribani watu wanne hujitoa kila siku kutokana na matatizo ya kawaida ya akili.

• Shirika la afya duniani limeonya kuwa vijana wa  chini ya umri 29 ndio wako katika hatari zaidi ya kujitoa uhai duniani.

Image: HISANI

Leo Jumanne, wizara ya afya inatarajiwa kuzindua  mwongozo wa kitaifa wa kliniki kwa ajili ya udhibiti wa matatizo ya kawaida ya akili kwa ushirikiano na shirika la vituo vya kudhibiti magonjwa (CDC) na washikadau wengine huku ulimwengu unapoadhimisha siku ya kuzuia kujitoa uhai duniani.

Mwongozo huo unalenga kuwapa wahudumu wa afya ujuzi na taarifa ya jinsi ya kutoa mafunzo ya afya ya akili yenye ufanisi na yenye msingi wa ushahidi.

Kulingana na takwimu za shirika na afya duniani WHO, inakadiriwa kuwa viwango vya watu kujitoa uhai nchini Kenya ni takribani watu wanne kila siku ikiashiria kuwa idadi ya watu wanaojitoa uhai ni 6.1 kwa 100,000.

Katika uchunguzi uliofanywa na taasisi ya taifa ya afya nchini Kenya mwaka wa 2023, sababu kuu nne zilibainika kuchangia idadi kubwa ya kujitoa uhai. Sababu hizo zilikuwa shida za kibinafsi na uhusiano, ugumu wa kifedha na kiuchumi, matatizo ya afya ya akili pamoja ushawishi wa kidini na utamaduni.

Kwenye utafiti huo huo, ilibainika kuwa Kenya inaongoza barani Afrika kwenye visa vya kujitoa uhai licha ya kuzidisha juhudi za kukabili kujitoa uhai haswa katika hatua za kubuni sera zinazolenga kuendeleza mikakati ya kuzuia kujiua kitaifa.

Hata hivyo, wizara ya afya imesema kuwa kujitoa uhai ni sababu ya tatu ya vifo katika vijana wa kati ya umri wa miaka 15 na 29.

Aidha WHO inaonya kuwa vijana wako hatarini zaidi ya kujiua.

View Comments