In Summary

•Katika taarifa ya Jumapili, KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, Machakos, Nandi, Kisumu, Migori, na Meru.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Septemba 16.

Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, Machakos, Nandi, Kisumu, Migori, na Meru.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mtaa wa Lower Kabete zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za Mombasa Road na Kinanie katika kaunti ya Machakos zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Mosoriot na Baraton katika kaunti ya Nandi yataathirika kati ya saa nne asubuhi na saa nane alasiri.

Eneo la Katito katika kaunti ya Kisumu litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Eneo la Macalder katika kaunti ya Migori pia litaathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Meru, maeneo ya Maua, Laare, na Garbatula yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

View Comments