In Summary

•Waziri wa uchimbaji madini na uchumi wa bluu,Ali Hassan Joho,ameamurisha kusimamishwa kwa uchimbaji madini ambao ni haramu.

•Aidha,Joho amesema kuwa watachukua  hatua za kisheria endapo walengwa watazidi kuendelea na shughli hiyo ya kudhalimu madini hayo 14.

ALI HASSAN JOHO.
Image: FACEBOOK

Waziri wa uchimbaji madini na uchumi wa majini, Ali Hassan Joho,ameamurisha kusimamishwa kwa uchimbaji haramu wa madini ili kuweka mikakati kabambe kwa uchimbaji madini.

Kwa taarifa ambayo imetolewa na wizara hiyo kutoka kwa ofisi ya gavana huyo wa zamani wa Mombasa,ambayo ni tarehe 14, septemba ,inasema kwamba wamewerza kugundua kuna baadhi ya watu ambao wandhalimu madini kama vile shaba,koltani na kromiti na ambayo yamechapishwa kwenye gazeti la kiserikali kimkakati.

Kulingana na taarifa hiyo,madini ambyo yamewekewa mikakati katika uchimbaji ni pamoja na grafiti,nikeli,lithum,Niobium,Tantalum,Thorium,Tsavorite,Tin Rare Earth na Urani.Madini hayo yalikuwa yamependekezwa na wizara hiyo manamo octoba 3, na kisha baadae yakachapishwa rasmi kwenye gazetui la kiserikali,uchimbaji wao kuwa wa kimkakati.

Aidha,Joho alisema kuwa shughli zozote ambazo zinahusisha utafutaji wa chimbo,uchimbaji,kupiga mnada na vile vile usindikaji wa madini hayo,ni lazima ufanywe kwa ushirikiano wa shirika la kitaifa la Uchimbaji madini(NAMICO).

Joho,vile vile alisema kuwa serikali kwa ushirikiano na wizara hiyo,hawatasita kutumia mkono wa sheria endapo baadhi ya watu wataendelea na kudhalimu madini hayo,huku akisema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwao.

Hatua hii itakuwa inalenga pakubwa kuzuia madini ambayo yakitiliwa mikakati kabambe katika uchumbaji yanaweza kufaidi pakubwa taifa.Kanuni hiii inaegemea chapisho la kiserikali mnamo Novemba 3,2023, ambalo linanuia kulinda madini adimu.

 

View Comments