In Summary

• Wabunge wa EAC wamelalamikia gharama ya juu ya kusafiri katika mataifa wanachama wa umoja wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

•Wanasema kuwa kuwepo mkwa mfumo mmoja wa usafiri wa anga utaongeza mapato la mataifa kutokana na safari za mara kwa mara.

Ndege ya Kenya Airways
Image: HISANI// KENYA AIRWAYS

Wabunge wa jumuiya ya Afrika mashariki wamependekeza kuwepo mfumo mmoja wa usafiri wa anga baina ya nchi wanachama.

Kulingana na wabunge hawa, usafiri huo utarahisisha gharama ya usafiri wa anga katika eneo lao.

Wabunge hao wanasema kuwa usafiri kwa kutumia ndege katika anga ya jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa ghali mno  kutokana na mataifa kutaka kukusanya kodi nyingi.

Pendekezo hilo kulingana na wabunge hao, wanasema kuwa litaongeza mapato ya nchi kutokana na usafiri mwingi ambao wananchi watafanya katika mataifa jirani.

Watunzi hao wa sheria walikubaliana kuweka mapendekezo hayo wakiwa katika mkutano wa  wakala wa uangalizi wa usalama wa anga (CASSOA) jijini Entebbe, Uganda.

Jumuiya ya Afrika Mashariki inajumulisha mataifa ya Somalia, Kenya, Tanzania, Uganda, Sudan Kusini, Rwanda, Burundi na Jmahuri ya Kidemikrasia ya Kongo.

Aidha CASSOA inashughulika na kuhakikisha miongozo ya uendeshaji wa usafiri wa anga kuwa zinahakiki viwango vya kimataifa. 

Pia CASSOA hutoa mwelekeo na usaidizi kwa washirika wa EAC kama kuweka mikakati ya ugavi wa rasilimali kwa wafanyakazi wa kiufundi.

View Comments