In Summary

• Kaimu IG Masengeli kupipitia wakili wake Cecil Miller na Steve Ogolla wamemwambia jaji wa mahakama ya juu Chacha Mwita kuwa mteja wao yuko tayari kufika mbele ya mahakama.

• Faili ya Masengeli iliwasilishwa mbele ya jaji Mwita kwa kuwa jaji Mugambi anawajibikia kesi nyingine inayoendeshwa na majaji watatu.

Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli. Picha: NPS/X

Kaimu inspekta jenerali wa polisi Gilbert Masengeli hatimaye amekubali kuheshimu amri ya mahakama na kufika mbele ya jaji Lawrence Mugambi Alhamisi 19.

Kupitia wakili wake Cecil Miller na Steve Ogolla, wamemuarifu jaji wa mahakama ya juu Chacha Mwita kuwa mteja wao yuko tayari kufika mbele ya kaoti kati ya saa 6 na 8 mchana.

Faili ya Masengeli iliwasilishwa mbele ya jaji Mwita kwa sababu jaji aliyemhukumu Masengeli kifungo cha miezi sita ambaye ni Lawrence Mugambi  alikuwa anajukumika katia keshi nyingine inayoendeshwa na majaji watatu akiwemo Mugambi.

Mawakili wa Masengeli waliiomba mahakama kumruhusu mteja wao kufika mbele ya mahakama leo kwa kuwa kifungo chake kitaanza rasmi Ijumaa tarehe 20.

"TUunaomba utupe mwelekeo ndio tuweze kufika mbele ya jaji Mugambi leo." Alisema wakili Miller.

Hata hivyo, jaji Chacha Mwita alielekeza faili ya Masengeli kuwasilishwa kwa jaji Mugambi Ijumaa asubuhi kwa maelezo zaidi.

View Comments