In Summary

• Wajumbe wa kamati hiyo walishangaa jinsi chuo kikuu kilivyolipa kiasi chote cha mkataba bila mkandarasi kumaliza ujenzi wa geti.

• “Unajenga lango la Ksh.24 milioni na bado huna mufilisi? Kuna nini kwenye lango hili, ni lango la ghorofa?" Mwenyekiti wa Kamati Wamboka aliuliza.

 

GETI LA MOI UNIVERSITY.
Image: HISANI

Watumizi wa mitandao ya kijamii wamegawanyika kwa maoni baada ya kubainika kwamba chuo kikuu cha Moi jijini Eldoret kilitumia takribani shilingi milioni 30 kwa ujenzi wa lango la kisasa.

Kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi wa matumizi ya fedha chuoni humo, ilibainika kwamba uongozi wa chuo cha Moi ulitoa zabuni ya Sh29.8m kwa ujenzi wa geti la kisasa katika chuo hicho.

Akizungumza alipofika mbele ya Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Umma kuhusu Elimu Jumatano, Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Moi Prof Isaac Kosgey alisema awali walikuwa na bajeti ya Ksh.4.8m, lakini hii ilitelekezwa kwa sababu lango lilikuwa kwenye hifadhi ya barabara.

Prof. Kosgey aliambia kamati inayoongozwa na Mbunge wa Bumula Jack Wamboka kwamba chuo kikuu kilitoa zabuni ya kujenga lango jipya kwa gharama ya Ksh.25 milioni, na kusababisha maswali ya ukaguzi.

"Tulilazimika kuacha mradi wa kwanza kwa sababu tulishauriwa na Mamlaka ya Barabara za Vijijini (KeRRA) kwamba lango lilikuwa kwenye hifadhi ya barabara," alisema Makamu wa Chansela.

Wajumbe wa kamati hiyo walishangaa jinsi chuo kikuu kilivyolipa kiasi chote cha mkataba bila mkandarasi kumaliza ujenzi wa geti.

“Unajenga lango la Ksh.24 milioni na bado huna mufilisi? Kuna nini kwenye lango hili, ni lango la ghorofa?" Mwenyekiti wa Kamati Wamboka aliuliza.

Kamati hiyo pia ilisikia jinsi wafanyikazi wa chuo kikuu walivyoelekeza mamilioni ya pesa zilizokuwa zikilipwa kama karo ya shule hadi akaunti ya kibinafsi ya benki.

Kulingana na ripoti ya ukaguzi, wafanyikazi hao walielekeza Ksh.7.7 milioni zilizokusudiwa kulipwa kwa Chuo Kikuu cha Moi katika akaunti yao ya Ustawi wa Chuo Kikuu cha Moi.

 

View Comments