In Summary

•Watu wawili wapoteza maisha yao kutokana na ajali ya barabarani katika barabara kuu ya Keroka-Masimba iliyohusisha lori na pikipiki.

•Polisi kutoka Masimba wamedokeza kuwa dereva wa lori husika alitoweka asijulikane aliko huku msako ukiendelea.

police car
Image: hisani

Watu wawili wamethibitishwa kufariki dunia baada ya kuhusishwa kwa ajali ya barabarani katika barabara kuu ya Keroka-Masimba iliyoko katika kaunti ya Kisii.

Wawili hao ambao ni wanaume, inasemekana walikuwa kwenye bodaboda kabla ya maisaha yao kukatizwa,waliaga hapo kwa hapo baada ya kugongwa na lori.

Kutokana na taarifa kutoka kwa polisi,inasemekana kuwa bodaboda hiyo,iligongana ana kwa ana na hiyo lori jambo ambalo lilipelekea kupoteza kwa maisha ya wawili hao.

Inasemekana kutokana na ajali hiyo,dereva wa lori hilo,alitoweka asijulikane aliko huku polisi wakidokeza yeyote atakaye muona kupiga ripoti kwao hili mkono wa kisheria kuchukuliwa juu yake.

Polisi kutoka Masimba waliichukuwa miili ya marehemu na kuipeleka kwenye makafani ya hospitali ya Keroka huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Ajali hii inatokea wakati Nchi imeshuhudia visa takriban 825 ambazo zimehusisha pikipiki takwimu za kutoka mwezi januari hadi septemba,aidha vifo 3369 zikitokea kwa ujumla na watu 1281 wakiwa ni watembea miguu.

 

View Comments