In Summary

•Mhadhiri huyo Dkt. Samwel Owino Mwanda alisemekana alikuwa amerejea nyumbani siku chache kutoka Nairobi.

• Mwili wake ulipatikana ukinining'inia mtini,huku akiwa ameacha kijikaratasi chenye nambari ya mkewe.

Image: HISANI

Polisi katika kaunti ya Homa Bay wameanza uchunguzi wa kubaini chanzo cha kifo cha mhadhiri mkuu wa chuo kikuu cha  Nairobi ambaye anayekisiwa huenda alijitia kitanzi katika mazingira ya nyumba yake kijiji cha Kachola,Kata ndogo ya Kodera kusini,eneo bunge la Rachuonyo.

Mhadhiri huyo Dkt. Samwel Owino Mwanda alisemekana alikuwa amerejea nyumbani siku chache kutoka Nairobi. Mwili wake ulipatikana ukining'inia kwa mti katika boma lake na mfanyikazi wake.

Kulingana na chifu wa Kodera kusini Joseph Mboga uchunguzi wa awali waonyesha kuwa  alijitia kitanzi na wako kwenye harakati za kubaini chanzo.

Kamanda wa polisi wa Homa Bay Hassan Barua, alithibitisha kisa hicho akisema kuwa  marehemu alipata chakula cha jioni na wafanyakazi wake na alitarajiwa kusafiri jijini Nairobi siku ya Ijumaa 20.

Aidha, Barua alisema kuwa walipata ngazi iliyokuwa kando na mti ambao mwili wake ulipatikana ukining'inia na kijikaratasi kilichokuiwa na nambari ya mke wake.

Mwili wa mwendazake ulipelekwa kwa makafani ya Rachuonyo, huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Kifo cha mhadhiri huyo kinajiri siku chache baada ya wahadhiri wa vyuo vikuu kutangaza mgomo kushinikiza serikali kutekeleza nyongeza ya mshahara wao pamoja na matakwa mengine. 

 

View Comments