In Summary

• Kikosi cha polisi wa Kenya nchini Haiti kimepiga hatua kubwa katika kurejesha utulivu kwenye ngome za magenge nchini humo.

• Kikosi hicho aidha kimelelamikia ucheleweshaji wa zana za vita kila wakati wanahitaji kukabiliana na magenge hatari.

Rais William Ruto alipozuru nchini Haiti mnamo 21 Septemba, 2024
Image: X// William Ruto

Maafisa wa polisi wa Kenya wanaondeleza urejesho wa amani na utulivu katika nchi ya Haiti wamelalamikia kuhusu maswala kadhaa wanayokumbana nayo katika opreseheni yao nchini humo.

Katika  kikao cha pamoja baina ya rais William Ruto na polisi hao,rais Ruto alitaka kufahamu matatizo wanayopitia maafisa hao  wakati wa wa operesheni zao'

Afisa mmoja alisema kuwa kuna chnagamoto nyingi wanapitia kazini ikiwemo kucheleweshwa kwa silaha wanazohitaji katika kupambana na magenge hatari ya Haiti.

Afisa huyo kwa jina Otieno alisema kuwa  mara nyingi zana za kivita wanazoitisha kutumia kukabiliana na magenge huchelewa kuwafikia kila wakati wanahitaji kuongezwa.

Otieno aliiombba serikali na mamlaka husika kushughulikia swala hilo haraka iwezekananvyo ili wananchi wa Haiti wapate usaidizi wa kibinadamu kwa wakkati unaofaa.

Vile vile maafisa hao wametaka taarifa kuhusu fidia waliyoaidiwa kuwekwa wazi angalau wawe na ufahamu wa jinsi fidia hiyo inatolewa.

Kwa kujibu hilo, rais Ruto alisema kuwa tayari polisi wa Kenya ambao wako Haiti wana bima ya afya chini ya huduma ya taifa ya polisi. Hata hivyo, rais Ruto aliwaahidi kuweka wazi taarifa ya fidia kupitia chaneli mwafaka wanazozifahamu.

Afisa mwingine alilalamikia kuwa baadhi yao bidhaa muhimu ikiwemo rasilimali za kivita zilibaki Kenya licha ya kuwa vifaa muhumu sana katika operesheni.Alimwomba rais kuhakikisha kuwa rasilimali hizo zinawafikia kwa wakati kurahisisha operesheni zao.

Aidha rais Ruto amesifia kikosi cha Kenya kuwa alipokea taarifa kuwa ngome kuu ya magenge hayo iliyokuwa chini ya Mkuu wa genge hilo Barbeque ilisalimu amri.

 

View Comments