In Summary

•Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kuitaka serikali kutoa mwelekeo mpya wenye uwazi kuhusiana na swala la uuzwaji wa uwanja wa ndege wa JKIA kwa shirika mla Adani.

•Aidha,kalonzo ameitaka seerikali kukusanya maoni ya wananchi kabla ya kuidhinisha makubaliano hayo,akisema swala hilo endapo litafaulu ,litawanufaisha viongozi wachache wa serikali na mwananchi wa kawaida kuhangaika.

KALONZO MUSYOKA
Image: HISANI

Kiongozi wa chma cha Wiper Kalonzo Musyoka sasa ametangaza njama ya kufungua mashtaka dhidi ya serikali kwa madai ya kuonekana kuwa kwenye makubaliano ya  bilioni $1.3 na shirika la Adani.

Kwenye makubaliano hayo, imedaiwa mikakati kama ujenzi wa mitambo ya kusambaza umeme na pia vile vile upanuzi wa kiwanja hicho cha ndege cha Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) na ambacho chenye shuguhli nyingi kwa taifa la Kenya.

Kalonzo, akizungumza wakati alipokuwa amehudhuria ibada ya kanisa katika kaunti ya Kajiado, alitoa hisia zake kuhusu njama fiche kwenye makubaliano hayo akisema makubaliano hayo yatanufaisha viongozi wachache wa serikali na kuwa mzigo kwa walipaji ushuru.

"maamuzi ya serikali kutofanya makubaliano na shirika la Adani kuwa wazi ni jambo ambalo linahibua maswali mengi na kuonyesha kutoaminika," Alisema Kiongozi huyo.

Aidha, alisema kuwa jambo hilo limetia wakenya wasiwasi akiwemo yeye kuhusu makubaliano hayo ya kisiri.

Aidha, Kalonzo aliituhumu shirika la Adani kwa makubaliano hayo kama chanzo kikubwa kwa ukosefu wa fedha ,akisisitiza kuwa makubaliano hjayo yatanufaisha viongozi wachache wa Serikali huku Mkenya wa kawaida akiteseka.

Kalonzo alisema kwamba yuko tayari kufungua mashtaka kunako tarehe 23 Septemba ili kusimamisha idhinisho la makubaliano hayo.Kando na hayo aliitaka serikali hasa wizara ya elimu sana kuangalia na kuujadili upya mfumo mpya wa kuwafadhili wanafunzi.Akisema kuwa mfumo huo utatilia kikomo kwa wanfunzi kupata ufadhili wa masomo ya juu.

"Mfumo huu mpya wa ufadhili umeleta mchanganyiko na kuwakosesha wanafunzi wenye haja ya ufadhili nafasi za kujiunga na vyuo vikuu". Alisema.

Kutokana na matamshi yake Kalonzo sasa joto linazidi kuonekana na kuleta upinzani kati ya shirika hilo na serikali,huku viongozi wengine waakitaka serikali kutoa mwelekeo wenye uwazi na kukusanya maoni ya wananchi kwa kufanya maamuzi.

View Comments