In Summary

•Seneta wa kaunti ya Makueni Dan Maanzo asema kuwa naibu rais hajafanya chochote kibaya na iwapo kuna mtu ambaye ameenda kinyume na katiba ni Rais mwenyewe.

•Aidha Maanzo alisema kuwa iwapo kuna mtu ambaye ameenda kinyume na katiba ni rais

DAN MAANZO
Image: HISANI

Seneta wa kaunti ya Makueni Dan Maanzo, amesema kuwa iwapo mswada wa kumtoa naibu rais Rigathi Gachagua  kwenye mamlaka utawasilishwa, lazima pia kuwasilishwe mwingine pia wa kumtoa rais Ruto.

Alisema maneno hayo wakati akihojiwa katika kituo kimoja cha televisheni cha humu nchini, tarehe 23 septemba.

"Kama wataleta mswada wa kumtoa mamlakani naibu rais,pia itabidi waaendae mwingine kumtoa mamlakani Rais Ruto, kwa sababu walichaguliwa kwa tiketi moja," Maanzo alisema.

Hili linakuja siku chache baada ya Naibu rais kusema kuwa ametolewa kwenye grupu ya Whatsapp ambayo shughli zote na matukio ya kiserikali uwekwa.

Aidha Gachagua alisema kuwa ni njama imepangwa ili ionekane kuwa yeye amedinda kufanya kazi na rais na pia shughli za kiserikali.

Aidha Maanzo alisema kuwa iwapo kuna mtu ambaye ameenda kinyume na katiba ni rais akisema kuwa endapo ni kutolewa mamlakani watatolewa wakiwea wawili.

"Kama kuna mtu ambaye ameenda kinyume na katiba ni rais mwenyewe, lakini si naibu wake...tutawafunga pamoja na kuleta mswada wa kuwatoa mamlakani wakiwa wawili kwa bunge la kitaifa na bunge la seneti,wathubutu kuleta mswada huo."

Aidha, maanzo alionekana kumtetea naibu rais akisema kuwa,"hakuna kitu kibaya ambacho naibu rais amefanya" aliendelea na kusema kuwa tishio la kuleta mswada wa kumtoa kwenye nafasi hiyo ya naibu rais ni jambo la kumtia kiwewe naibu rais Gachagua.

Hili linakuja siku moja baada ya katibu mkuu wa chama cha UDA, Cleophas Malala kusema kuwa watu wanafaa kupuuzilia mbali madai ya mswada wa kumtoa mamlakani naibu rais.

View Comments