In Summary

• Watekaji nyara waliwataka mtoto wa wake na shemeji wake kuwaelekeza nyumbani na walipofika waliwakosa waliokuwa wanawatafuta.

• Madai ya utekaji nyara kutoka kwa Malala yanajiri siku moja baada ya kiongozi huyo kuandamana na naibu wa rais Rigathi Gachagua katika hafla ya kanisa.

Ailyekuwa seneta wa Kakamega Cleophas Malala
Image: Facebook

Aliyekuwa seneta wa kaunti ya Kakamega Cleophas Malala, amedai kuwa mtoto wake na shemeji wake wa miaka 19 walitekwa nyara na baadaye kuachiliwa.

Kupitia ukurasa wa X, seneta huyo wa zamani ameandika kuwa mwanawe na shemeji wake walitekwa nyara kwa mtutu wa bunduki.

Malala amekiri kuwa baada ya kutekwa nyara kwa familia yake, waliteswa kwa takribani saa sita, watekaji nyara wakiwataka kuelezea alipo ama mke wake.

Kulingana na Malala, watekaji nyara waliwataka mtoto wa wake na shemeji wake kuwaelekeza nyumbani na walipofika waliwakosa waliokuwa wanawatafuta.

Hatimaye, shemeji wa Malala na mtoto waliwachwa katika barabara ya Thika ambapo Malala anadai kuwa aliwachukua mwenyewe.

Madai ya utekaji nyara kutoka kwa Malala yanajiri siku moja baada ya kiongozi huyo kuandamana na naibu wa rais Rigathi Gachagua katika hafla ya kanisa mjini Thika kaunti ya Kiambu.

Katika ibaada hiyo ya kanisani, Malala alikiri kuwa chama tawala cha UDA kimeondoka katika mwelekeo uliokusudiwa na chama hicho wakati wa kampeni.

Malala alisema kuwa ndoa ya chama cha UDA ina misukosuko baada ya baba wa boma hilo kuamua kuoa mke wa pili na sasa mke wa pili anataka kumfurusha mke wa kwanza.

Kwa muktadha wa Malala, baba wa boma la UDA ni rais William Ruto na mke akiwa naibu wa rais Rigathi Gachagua. Mke wa pili aliyekubaliwa kuolewa na baba wa UDA ni mwafaka uliowaleta baadhi ya viongozi wa upinzani katika serikali ambayo ndio ndoa ya serikali ya UDA.

View Comments