In Summary

• Maoni ya mbunge huyo yanafuatia maandamano huko Mumias Mashariki dhidi ya uamuzi wa mahakama, ambapo wakaazi waliangazia hatua za kimaendeleo zinazowezeshwa na NG-CDF.

MP SALASYA
Image: FACEBOOK

Mbunge wa Mumias Mashariki (Mbunge) Peter Salasya amewaonya vijana wa Gen Z kuhusu madhara yanayoweza kutokea iwapo wataunga mkono uamuzi wa hivi majuzi wa Mahakama Kuu ya kutangaza Sheria ya Kitaifa ya Hazina ya Maendeleo ya Serikali na Eneobunge (NG-CDF) ya 2015 kuwa kinyume na katiba.

Katika taarifa kwenye ukurasa wake wa Instagram mnamo Jumanne, Septemba 24, 2024, Salasya alielezea utayari wake wa kuungana na tabaka la kisiasa ikiwa Gen Zs wataendelea kutetea kukomeshwa kwa shughuli za NG-CDF.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, vijana hao ndio wanashinikiza kuondolewa kwa NG-CDF mikononi mwa wabunge na endapo hawatakataa kundolewa kwakwe, basin aye atawajibu kwa kuondoa uungaji mkono wake kwao.

“Jimbo la Mumias East wamekataa ujinga na huo ndio msimamo wangu kama kiongozi wao. Wenye hawajasoma sana wanaweza kuona madhara ya ngcdf lakini ni wachache wenye wivu ambao ni wasomi wasioweza kuchangia 1k kwa shule kwani wazazi kujenga vyoo au madarasa chakavu hawawezi kuyaona,” alisema.

“Ikiwa msimamo wa gen z ni kujitoa ngcdf kutoka kwa mwananchi wa ground .Nitaondoa uungwaji mkono wangu kwao na kujiunga na tabaka la kisiasa litakaloungana kuwatawala wanavyotaka. Gen z lazima tuwe wakweli hata pale kk gvt imeshindwa na ahadi zake za hosepipe atleast kupitia cdf yao ni matumaini madogo kwa watu wetu kupitia maendeleo na ni 56B tu nchi nzima,’ aliongeza.

Maoni ya mbunge huyo yanafuatia maandamano huko Mumias Mashariki dhidi ya uamuzi wa mahakama, ambapo wakaazi waliangazia hatua za kimaendeleo zinazowezeshwa na NG-CDF.

Kulingana na wenyeji, shule na biashara katika eneo hilo zimenufaika sana na hazina hiyo, ambayo wakaazi wanahoji kuwa imekuwa muhimu kwa ukuaji wa jamii.

Wakazi ambao walipinga uamuzi wa mahakama walionyesha wasiwasi kuhusu uwezekano wa kushindwa katika miradi ya maendeleo inayofadhiliwa kupitia NG-CDF.

View Comments