In Summary

•Wakaazi wa Eastlands sasa wameitaka serikali kuingilia kati na kuweka njia madhubuti za kuzuia ongezeko la panya na mende ambao wamekuwa wakiwaangaisha wakaazi hao.

•Wakaazi hao wameshtumu wauza vyakula vibandani kuchangia kwa kutupa mabaki ya vyakula ovyo ovyo na kuchangia pakubwa ongezeko la panya na mende.

Mende
Image: HISANI

Wakaazi wa maeneo ya Eastlands jijini Nairobi sasa wamatoa wito kwa serikali kuwasaidia kudhibiti panya na mende ambazo zimekuwa zikiwaangaisha kwenye maeneo yaom ya makaazi hususan kwenye nyumba zao.

Kulingana na wakaazi hao,walisema kuwa panya na mende hjao wanatokea kwenye mashimo ambayo yako wazi kutoka kwa njia ya maji taka na pia vile vile mashimo ambayo yamechimbwa eneo hilo kwa shughli za binadamu.

Wakizungumza na wanahabari wakaazi hao walisema kuwa kwa sasa wanahangaika baada ya panya na mende kuvamia nyumba zao kwa kutafuta chakula.

Akizungumza Phoebe Naliaka,mkaazi wa Embakasi,alisema,"Hivi majuzi nilipata panya mkubwa zaidi jikoni,ilibidi nikitupe chakula ambacho nilikuwa nimekipika kwakuwa nilihofia huenda panya huyo amekichafua".

Aidha,sasa wakaazi hao wameitaka serikali kuingilia kati na kuwasaidia ili kukinga ongezeko zaidi la panya na mende ikiwemo kupulizia dawa ambayo itazuia kuongezeka kwa viumbe hao.

Aidha wakazi hao walisema kuwa hapo awali serikali ilikuwa inapuliza dawa kwa mtaa huo lakini kwa sasa wamesusia shughli hiyo ambayo ni muhimu.

"Kwa muda uliopita tulikuwa tunaona wapuliziaji dawa wakipuliza dawa kila mtaa,hasa vichaka vidogo na pia mitaro,hili kumaliza mbu na wadudu wengine,lakini kwa sasa hawapo tena", Timothy Karanja kutoka Kaloleni alisema.

Wakaazi hao aidha vile vile walisema kuwa ongezeko la panya na mende katika mtaa huo limechangiwa pakubwa na utupaji takataka usikuwa na mipango na vile vile njia mbaya za maji taka.Wengine pia walilaumu pakubwa kuwa na vibanda vya kuuza vyakula ambapo wauzaji utupa mabaki ya chakula ovyo ovyo.

Kwa sasa, wakaazi hao wameitaka serikali hasa serikali ya kaunti kuwaajiri vijana ili kuondoa vichaka vidogo, kupulizia dawa kufungua njia ya maji taka mahali ambako imekwama.

View Comments