In Summary

• Uamuzi wa kufunga chuo hicho ulitolewa na seneti ya chuo hicho baada ya wanafunzi kufanya maandamano nje ya shule hiyo katika eneo la Gitunduti

• Shughuli za masomo zimeathirika katika vyuo vikuu vya serikali kutokana na maandamano ya wanafunzi kupinga mfumo wa ufadhili wa masomo uliotolewa na serikali.

Image: Hisani

Usimamizi wa chuo kikuu cha Karatina umekifunga ghafla chuo hicho kwa muda usiojulikana.

Uamuzi wa kufunga chuo hicho ulitolewa na seneti ya chuo hicho Jumatano mchana baada ya wanafunzi kufanya maandamano nje ya shule hiyo katika eneo la Gitunduti takribani kilomita moja kutoka chuo hicho. 

Kufuatia kufungwa huko, masomo ya muhula wa kwanza katika mwaka wa masomo 2024/2025 imeahirishwa.

Wanafunzi kupitia memo iliyotolewa na usimamizi wa chuo wametakiwa kuondoka katika makao ya chuo hicho kufikia saa tisa adhuhuri na kuhakikisha kuwa wale wanaoishi katika bwenio za shule wanatafuta makao mbadala kufikia wakati huo.

Seneti ya Chuo kikuu cha Karatina aidha imesema kuwa tarehe kamili ya chuo hicho kufunguliwa tena itatangazwa baadaye.

Katika siku za hivi karibuni shughuli za masomo zimeathirika katika vyuo vikuu vya serikali kutokana na maandamano ya wanafunzi kupinga mfumo wa ufadhili wa masomo uliotolewa na serikali.

Vile vile, wahadhiri wa vyuo vikuu wamesusia kuingia madarasani kufunza wakilalamikia serikali kutowajibikia mkataba waliokubaliana na chama cha kutetea maslahi ya wahadhiri (UASU)  wa mwaka 2021 hadi mwaka 2025.

 

View Comments