In Summary

• “Makutano haya ya matatizo yanaangazia udharura wa kuongeza uingiliaji kati wa kimataifa ili kukabiliana na udhaifu uliokithiri unaokabili makundi haya,” Ruto aliongeza.

RAIS WILLIAM RUTO
Image: FACEBOOK//RUTO-WILLIAM

Rais William Ruto ameuthibitishia ulimwengu kwamba maambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini bado ni kero kubwa haswa kwa makundi ya wanawake na vijana wa umri wa balehe.

Akizungumza Jumanne wakati wa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu "Multilateralism Works: Uongozi na Kudumisha Makabiliano dhidi ya UKIMWI kufikia 2030 na Zaidi" huko New York, Ruto alifichua kwamba Kenya sasa inakaribia kufikia udhibiti wa janga, baada ya kufikia malengo ya kimataifa ya 95-95-95.

Hata hivyo, rais alifichua kwamba janga la UKIMWI bado ni changamoto kubwa kwa kina mama, wasichana na vijana wa balehe kutokaka na kile alisema ni kutokuwepo kwa usawa wa ufikiaji wa matibabu nchini.

“Janga hili linaendelea kuathiri vibaya vikundi vilivyo hatarini, pamoja na wanawake, wasichana, vijana wa balehe, na idadi kubwa ya watu, ikichochewa na ukosefu wa usawa wa kiafya, unyanyapaa na ubaguzi,” rais alisema.

“Makutano haya ya matatizo yanaangazia udharura wa kuongeza uingiliaji kati wa kimataifa ili kukabiliana na udhaifu uliokithiri unaokabili makundi haya,” Ruto aliongeza.

Kwa mujibu wa hotuba hiyo ya rais, Hivi sasa, asilimia 95 ya watu wanajua hali zao za HIV, huku asilimia 102 ya waliogunduliwa wakiwa katika mpango wa kupokea matibabu, na asilimia 97 ya wale wanaopata matibabu wamefanikiwa kukandamiza virusi hivyo.

“95% ya watu wanajua hali zao za HIV nchini Kenya, 102% ya wale waliogunduliwa na virusi wanapokea matibabu na 97% ya wale waliotumia dawa wamefanikiwa kukandamiza virusi hivyo,” rais alithibitisha.

Hata hivyo, rais alisema kwamba tangu mwaka 2013, idadi ya vifo kutokana na UKIMWI nchini imepungua kwa 65%.

View Comments