In Summary

• Mhasibu na mhifadhi wa misitu wanadaiwa kupokea rushwa kwa kuwalipa wafanyakazi mshahara zaidi ya kiwango kinachohitajika kisha kudai kurejeshwa nyongeza ya juu.

• EACC inaendelea na uchunguzi ikidaiwa wawili hao hugawanya shilingi hizo na wakubwa wao kazini.

Wafanyakazi wawili wa idara ya huduma za misitu nchini wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Garissa baada ya  kupatikana wakihusika na ulaghai wa pesa za umma.

Wawili hao kwa majina Elphas Tembu Wesonga ambaye ni mhifadhi nwa misitu na Ibrahim Aden Hussein anayehudumu katika nafasi ya uhasibu, walikamatwa  katika msako uliofanywa na maafisa wa EACC  Jumanne tarehe 24.

Taarifa ya EACC imesema kuwa wawili hao wamekuwa  wakitekeleza mpango wa ulaghai kutumia wafanyakazi wengine wa shirika hilo la huduma ya misitu  katika eneo hilo.

EACC imebaini kuwa Elphas Wesonga na Aden Hussein wamekuwa wakiwalipa wafanyakazi wa kawaida mshahara zaidi wa kiwango kinachohitajika na kisha baadaye kuwashurutisha kutoa pesa ya ziada na kuwakabidhi.

Kulingana na EACC, pesa za ziada wanazolipwa wafanyakazi hurejeshewa washukiwa hao kwa matumizi yao ya kibinafsi.

Katika kamata kamata za EACC, takribani shilingi 73,000 zilipatikana kutoka kwa wafanyakazi wa kawaida wa huduma ya misitu siku hiyo.

Inadaiwa kuwa pesa zinzokusanywa na washukiwa hao hugawanywa baina yao na baadhi ya maafisa wengine juu yao.

 

View Comments