In Summary

•PSC ilitangaza kuwa kuna nafasi 42 za Makamishna Wasaidizi wa Kaunti II chini ya wizara ya Usalama wa Ndani na Utawala wa Kitaifa.

•Kwa maelezo zaidi ya nafasi zilizo wazi na utaratibu wa maombi, PSC iliwataka watu wanaopendezwa kufikia tovuti ya Tume.

Image: PSC

Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) imetangaza nafasi za kazi 144 katika wizara na idara mbalimbali za serikali.

Katika notisi iliyochapishwa kwenye jarida la My Gov mnamo Jumanne, Agosti 20, PSC ilitangaza kuwa kuna nafasi 42 za Makamishna Wasaidizi wa Kaunti II chini ya wizara ya Usalama wa Ndani na Utawala wa Kitaifa.

Tume pia inataka kuajiri maafisa 7 chini ya Idara ya Magereza na mkurugenzi mmoja wa uhamasishaji wa rasilimali katika idara ya hazina ya kitaifa.

Watu 22 wataajiriwa kuchukua kazi mbalimbali katika wizara ya Maendeleo ya Biashara Ndogo, Ndogo Kiasi na za Kiwangi cha Kati.

Katika idara ya serikali ya Utumishi wa Umma, maafisa 48 wataajiriwa kuchukua majukumu mbalimbali.

PSC pia inatafuta watu 13 kujaza nafasi mbali mbali katika idara ya masuala ya Bunge, watu 4 katika idara ya uchukuzi, na mtu mmoja katika idara ya Masuala ya Vijana na Uchumi wa Ubunifu.

Maafisa 5 pia watateuliwa kuchukua majukumu mbalimbali katika idara ya Umwagiliaji Maji.

Manaibu chansela wawili pia wanahitajika kuchukua majukumu katika Chuo Kikuu cha Chuka na Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Dedan Kimathi.

Kwa maelezo zaidi ya nafasi zilizo wazi na utaratibu wa maombi, PSC iliwataka watu wanaopendezwa kufikia tovuti ya Tume.

Watu wanaovutiwa na waliohitimu wanatakiwa kutuma maombi yao mtandaoni kupitia tovuti ya Tume: www.publicservice.go.ke au tovuti ya kazi: www.psckjobs.go.ke.

PSC ilisema maombi hayo yanafaa kufika kwa tume hiyo mnamo au kabla ya Septemba 10, 2024, saa kumi na moja jioni.

View Comments