In Summary
  • Hata huku maafisa wa polisi wakijaribu kumfariji ili atulie, mwanamume huyo hangesikia lolote
Jamaa aliyesababisha taharuki bungeni huku akidai kwamba ni mjukuu wake hayati Mwai Kibaki
Image: EZEKIEL AMING'A

Mwanamume anayeomboleza amezua taharuki katika majengo ya Bunge jijini Nairobi ambapo mwili wa rais mstaafu Mwai Kibaki umelazwa.

Mtu huyo ambaye hakutambuliwa alidai kuwa yeye ni mjukuu wa mbali wa marehemu Mwai Kibaki, na alihuzunishwa sana na taarifa za kifo chake.

"Kwa nini umeenda haraka sana," alisema, huku akitokwa na machozi.

Hata huku maafisa wa polisi wakijaribu kumfariji ili atulie, mwanamume huyo hangesikia lolote.

“Niruhusu nimwone kwa mara ya mwisho,” aliwaambia maafisa hao.

Mwanaume huyo alitangulia kuvua baadhi ya nguo zake, akipinga aruhusiwe kuutazama mwili wa ‘babu yake’ aliyeanzisha elimu ya msingi bila malipo.

Baadaye maafisa wa polisi walimsindikiza mwanamume huyo kutoka kwa Majengo ya Bunge baada ya juhudi za kumtuliza kutozaa matunda.

Image: EZEKIEL AMING'A

Mwili wa rais mstaafu Mwai Kibaki uliwasili katika Majengo ya Bunge jijini Nairobi kutoka makafani ya Lee Jumanne asubuhi kwa siku ya pili ya kutazamwa na umma.

Wakenya ambao hawakuutazama mwili wa Mwai Kibaki siku ya Jumatatu sasa watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.

Mwili wa Rais mstaafu Kibaki utaagwa kutoka Jumatatu hadi Jumatano.

Wakati huu, umma utaruhusiwa kuutazama mwili huo kabla ya Mazishi ya Kiserikali siku ya Ijumaa katika uwanja wa Nyayo.

 

 

View Comments