In Summary
  • Mwanadada asimulia alivyokejeliwa na wakwe wake kwa kuwa tasa
  • Hamna mwanamke ambaye hatamani kuwa na mtoto kila mmoja anatamani, lakini kwa wakati wake Mungu."
sad woman

Kila mwanamke hutamai kwamba akiolewa na mpenzi wa maisha yake wakwe wake watamkaribisha na kumpenda kama mtoto wao.

Kuna baadhi ya wanawake matarajio na matumaini yao hugeuka kuwa ndoto baada ya kupatana na wakwe ambao hawamhitaji.

Pia kuna wale waamebahatika na kuwapata wakwe wenye nidhamu na wazuri, kuliko matarajio yake.

Nikiwe kwenye Ziara Yangu nlipatana na Jacinta ambaye alifunga ndoa yake mwaka wa 2016.

KUlingana naye amekuwa akimtafuta kumpata mtoto lakini hajafanikiwa.

Uchungu zaidi amekumbuka jinsi alivyotoroshwa na wakwe wake kwenye boma lake na kumtafutia mumewe mwanamke mwingine.

"Nilifunga pingu za maisha na aliyekuwa mume wangu mwaka wa 2016, tumekuwa tukimtafuta mtoto bila mafanikio yeyote mapema mwaka uliopita wakwe zangu waliamua kumtafutia mume wangu mke mwingine kwani walisema kwamba mimi ni tasa na siwezi zaa

Kitu ambacho kiliniuma kama mwanamke ni kuwa dada wa mume wangu walikuwa kwennye mstari wa mbele kunifukuza na kuniambia kwamba nitakufa kama mbwa mwitu, kwani siwezi barikiwa na mtoto

Walinikejeli kila kuchao hata sikuwa na amani kwenye ndoa yangu, lakini niliamua kujipenda na kuachana na mambo ambayo yangeweza kunipa msongo wa mawazo, ndio nilipata msong wa mawazo lakini nilimuona mtaalamu na hayo yakapita, ndio huwa wanasema utamu wa ndoa ni mtoto, lakini mume wangu hakusema chochote nilipokuwa nakejeliwa, nasubiri tu majaliwa ya wenyezi Mungu

Hamna mwanamke ambaye hatamani kuwa na mtoto kila mmoja anatamani, lakini kwa wakati wake Mungu."

 

 

 

 

 

 

View Comments