In Summary
  • DCI yafichua kwa nini hawatoi matukio ya kusisimua yaliyofanyika Naivasha
Image: JACK OWUOR

Baada ya kuahidi kutoa ripoti ya kina kuhusu drama iliyotokea Naivasha wakati wa Safari Rally wikendi, DCI amebatilisha kazi hiyo baada ya mkuu wa DCI George Kinoti kuingilia kati.

Timu ya mawasiliano ya DCI ilikuwa imeahidi kutoa kila undani wa kile kilichotokea Naivasha, lakini kwa minajili ya amani katika ndoa, wameghairi kumwaya mtama huo.

Kwenye mitandao ya kijamii, DCI ilibaini kuwa walikuwa na uzi wa kina wakisimulia jinsi drama  zilivyotokea, lakini kabla ya kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii, bosi wa DIC Kinoti aliingilia kati na kusitisha misheni hiyo.

DCI ilibainisha kuwa Wakenya wengi wangemwaga machozi ikiwa wangetoa ripoti hiyo na kwamba ndoa nyingi zingeweza kuvunjika kabla ya wakati wake.

"Vinginevyo mkuu Kinoti amesema tukanyagie hadithi hiyo ya Vasha. Vile admin hajalala akiunda thread, ingekuwa premium tears. Ndoa zingevunjika. Ama tupatie," Timu ya mawasiliano ya DCI ilibainisha.

View Comments