In Summary
  • Mmiliki wa tikiti ya Jubilee alifichua kuwa pia aliahidiwa kazi
  • Bahati alisema hawezi kuhujumiwa akidai ndiyo sababu wapinzani wake wamebuni njia nyingine za kumwangusha
Msanii Bahati Kelvin Bahati Kioko anayelenga ubunge Mathare kupitia chama cha Jubilee
Image: Instagram screenshot

Msanii wa Kenya Kelvin Bahati Kioko anadai alipewa Sh50m kuacha kinyang'anyiro cha ubunge cha Mathare.

Akizungumza na Radio Citizen siku ya Jumatano, Bahati alisema wapinzani wake wamekuwa wakimpigia debe ajiuzulu.

“Wamenipatia mamilioni hadi Sh50 milioni wanajua wakifika ofisini watapata fedha,” alisema.

Mmiliki wa tikiti ya Jubilee alifichua kuwa pia aliahidiwa kazi.

“Lakini sitafuti kazi, najitafutia riziki kutokana na muziki wangu,” alisema.

Bahati alisema hawezi kuhujumiwa akidai ndiyo sababu wapinzani wake wamebuni njia nyingine za kumwangusha.

Alimtaja mbunge aliyeko madarakani Anthony Oluoch kuwa mmoja wa waliofika kwake kuomba uungwaji mkono.

"Aliniambia nimfanyie wimbo wa kampeni na kumuunga mkono. Wanataka kumtumia mtu wa Mathare kufika kwa watu."

Bahati alisema anajuta kwamba katika nyanja ya siasa, mtu hawezi kuwa na marafiki anaoweza kuwaamini.

"Ninakosa marafiki wa kweli, katika siasa, unakaa na rafiki yako ambaye anasema wasichomaanisha. Wanasiasa wengi sio wa kweli."

 

 

View Comments