In Summary

• Katika picha na video ambazo zimepakiwa kweney mitandao ya kijamii, makumi ya maafisa wa kulinda usalama kutoka vitengo vyote wameonekana wakipiga doria karibu na maeneo hayo.

Huku taifa likisubiria kwa hamu kuu uamuzi wa mahakama ya upeo mchana wa Leo katika kei iliyowasilishwa na muungano wa Azimio na watu wengine wakilenga kutaka kubatilishwa kwa ushindi wa William Ruto, ulinzi mkali umeonekana nje na karibu na maeneo ya mahakama kuu ya Milimani ambako uamuzi huo utatolewa.

Jopo la majaji saba linatarajiwa kukongamana adhuhuri katika mahakama hiyo ili kuwataarifu Wakenya mbivu na mbichi kuhusu kesi inayopinga uchaguzi ulioendeshwa Agosti 9 na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Katika picha na video ambazo zimepakiwa kweney mitandao ya kijamii, makumi ya maafisa wa kulinda usalama kutoka vitengo vyote wameonekana wakipiga doria karibu na maeneo hayo.

Ikumbukwe Jumapili jioni idara ya polisi ilitangaza kwamba baadhi ya barabara zinazoelekea katika maeneo ya mahakama ya Milimani zitasalia kufungwa siku ya leo.

Katika moja ya video, polisi walinda usalama wanaonekana wakipiga doria kwa farasi wengine wakiwa na magari ya kuwatawanya watu kwa maji ya kutoa machozi.

 

View Comments