logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+videos) Baba na bintiye wafukuzwa katika jamii kwa kuzaa watoto 2 pamoja

Mzee huyo asiye na aibu alieleza kwamba alimlisha bintiye Yamini ya kuwa mke wake kwa sababu hakuwa anataka amuache na kuondoka kama ambavyo mke wake aliondoka.

image
na Radio Jambo

Makala10 September 2022 - 10:15

Muhtasari


• Alisema kwamba mke wake baada ya kuondoka na watoto wengine, aliamua kumlisha kiapo msichana huyo ili naye asitoroke na kumuacha katika upweke.

Jamii moja nchini Nigeria imemfukuza baba na bintiye baada ya kuoana na kuzaa watoto wawili pamoja kama mume na mke.

Katika video ambapo imepakiwa kwa sana mitandao ya kijamii, mwanadada huyo kwa jina Queen Bassey anasemekana kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na babake mzazi kipindi mamake alitoroka.

Mwanadada huyo ambaye baada ya kugundulika na wana jamii walijawa na hasira walimhoji na kueleza kwamba babake ndiye aliyemvunja ubikra na wakaanza kuishi na yeye kama mke na mume. Alisema kwamba hawezi kueleza ni kwa nini aliruhusu kitendo hicho cha aibu kufanyika kati yake na babake mpaka kuzaa watoto wawili na yeye.

Wana jamii wenye ghadhabu ilibidi wamtafute babake msichana huyo na kumkebehi kwa kitendo hicho alichofanay kwa binti yake.

Mzee huyo aliyetambulika kwa jina Agnalasi alipopatwa na kuwekwa chini ya ulinzi na wana kitaa wenye mshangao mkubwa uliochanganywa na hasira, alishinikizwa na hatimaye akafunguka sababu zake kufanya hivyo.

Mzee huyo asiye na aibu alieleza kwamba alimlisha bintiye Yamini ya kuwa mke wake kwa sababu hakuwa anataka amuache na kuondoka kama ambavyo mke wake aliondoka.

Alisema kwamba mke wake baada ya kuondoka na watoto wengine, aliamua kumlisha kiapo msichana huyo ili naye asitoroke na kumuacha katika upweke.

Duniani matukio ni mengi, mengine ya kushtusha, kufurahisha na mengine ya kuchefua roho.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved