Kwa mara ya kwanza katika maisha yake, William Ruto amepanda gari la sherehe rasmi za kitaifa na kuzungushwa katika uwanja wa Kasarani akiwapungia watu mkono kwa furaha kubwa.
Gari hilo kwa kawaida hutumiwa na rais aliye madarakani na itakumbukwa rais Kenyatta aliingia katika uwanja huo wa Kasarani akiwa katika gari hilo huku akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamejawa na mbwembwe, lakini baada ya kumkabidhi Ruto madaraka, aliondoka kwa msafara wake rasmi huku gari hilo likibaki kutumiwa na Ruto kwa mara ya kwanza kuwapungia watu mkono.
Hapa tunakuandalia baadhi ya picha za tukio hilo la kihistoria si tu kwa taifa la kenya bali pia katika maisha ya Ruto.