logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mlinzi wa jeneza la malkia Elizabeth II azimia na kuanguka chini (+video)

Wanajeshi waliandamana na jeneza kutoka Buckingham Palace kuelekea Westminster ambapo mmoja wao alidondoka na kuzimia ghafla.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri15 September 2022 - 11:54

Muhtasari


• Ilitokea wakati kundi la walinzi wakianza kubadilishana majukumu na mmoja alionekana kutetemeka kabla ya sekunde chache kuanguka - Mirror waliripoti.

Malkia Elizabeth wa pili aliendelea kuombolezwa baada ya kifo chake wiki jana.

Mwili wa malkia huyo wa muda mrefu wa Uingereza wiki hii ulilazwa katika eneo la Westminster kwa umma kutoa heshima za mwisho kwake huku walinzi wakiwa wanaulinda usiku na mchana.

Katika video moja ambayo imekuwa ikisambazwa kweney mitandao ya kijaa, mlinzi mmoja anaonekana akipoteza fahamu na kuanguka chini huku umati ukiwa unazidi kupanga foleni kuutazama mwili wa Malkia Elizabeth.

“Wanajeshi waliandamana na jeneza kutoka Buckingham Palace siku ya Jumatano lakini kwa mmoja wa walinzi katika Ukumbi wa Westminster dhiki ilionekana kuwa nyingi sana kwani alizimia ghafla. Kulikuwa na miguno kutoka kwa waombolezaji alipokuwa akianguka chini ambayo ilinaswa kwenye video. Ilitokea wakati kundi la walinzi wakianza kubadilishana majukumu na mmoja alionekana kutetemeka kabla ya sekunde chache kuanguka,” jarida la Mirror nchini Uingereza liliripoti.

Maafisa wawili wa polisi walionekana wakikimbia kumchukua kabla ya video kukatwa na kisha kwenda kwenye picha za Mabunge.

Watazamaji walioshtushwa pia waliingia kwenye mitandao ya kijamii na ujumbe mmoja wa Twitter: "Lazima amelemewa sana na kile kilichokuwa kikitokea."

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved