In Summary

• “Hii mpe tu mwanafunzi wa ndani katika kampuni yako ya uwakili ☺️ - hii ni hewa moto,” mmoja kwa jina Gathuki Ngahu alisema.

Mutula Kilonzo Jr Gavana wa Makueni apuuzilia mbali kesi ya kupinga ushindi wake.
Image: Facebook

Gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Jr amekejeli ombi lililowasilishwa mahakamani na aliyekuwa mshindani wake katika kinyang’anyiro cha ugavana, Patrick Mweu Musimba.

Musimba alikuwa ni mbunge wa Kibwezi West kabla ya kuingia debeni akilenga kumrithi gavana aliyemaliza hatamu yake ya miaka kumi, profesa Kivutha Kibwana.

Katika barua ya kesi hiyo ambayo iliwasilishwa katika ofisi ya Mutula Kilonzo ikimtaja kama mshtakiwa kwenye kesi hiyo, Musimba pia alitaja tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Katika kile kilichoonekana kama kuipuuzilia mbali kesi hiyo, gavana Kilonzo Jr alipakia barua hiyo na kuifuatisha kwa maneno ya chekechea yaliyotajwa kwenye mahakama ya upeo wiki juzi na wakili Willis Otieno, “Piki Piki ponk paka mielo disco.”

Katika uchaguzi wa Agosti 9, Mutula Kilonzo Jr alipaka kura nyingi mno zaidi ya laki mbili huku Musimba ambaye alikuwa mshindani wake mkuu akipata kura takribani elfu 60 tu, na sasa amewasilisha kesi kupinga kuchaguliwa kwa Kilonzo Jr kwa kile anasema shughuli ya uchaguzi ilikumbwa na dosari chungu nzima.

Baada ya Kilonzo Jr kupakia barua hiyo na kuikejeli kwa maneno ya wakili Willis Otieno, watu wengi walionekana kutolea maoni kwamba Musimba alikuwa anajiabisha bure kwani hata kura alizoshindwa nazo ni nyingi mno.

Wengine walimtaka Kilonzo Jr kuwatuma mawakili wachanga katika kampuni yake ya mawakili ili kumwakilisha kwani kwa hadhi yake hahitaji kabisa kujiwakilisha katika kesi hiyo yenye walisema haina mashiko.

“Hii mpe tu mwanafunzi wa ndani katika kampuni yako ya uwakili ☺️ - hii ni hewa moto,” mmoja kwa jina Gathuki Ngahu alisema.

“Bwana mkuu wa kaunti unaonekana kuonyesha kuwa mlalamishi anajishughulisha na kukimbizana na bata bukini wa mwituni,” Mwalimu Katebes Kibet alitania.

“Nashuka pale nione ni nani huyu anayepuliza hewa moto na kukimbiza bata bukini mwitu huko Makueni, hakuna anayeweza kushindana na Mutula Junior sio Makueni tu bali hata Ukambani. Ngoja tusubiri tuone ataenda wapi,” Charles Kilonzo alisema.

 

View Comments