In Summary

• Akombe alipakia picha hiyo akidokeza kurudi Ethiopia baada ya ziara kusini na magharibi mwa Afrika mtawalia.

Miguna Miguna afurahia uvaaji wa Roselyne Akombe
Image: Twitter

Aliyekuwa kamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Roselyne Akombe amepongezwa kwenye mtandao wa Twitter na wakili Miguna Miguna kwa uvaaji wake mzuri.

Akombe alipakia picha akiwa kwenye ngazi za nyumba akidokeza kwamba ndio mwanzo alikuwa amerejea katika jiji la Addis Ababa Ethiopia kutoka ziara mbali mbali.

Akombe alitoroka nchini mnamo mwaka 2018 baada ya muungano wa NASA kipindi hicho ukiongozwa na Raila Odinga kupinga vikali matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2017 na kuwa na msisitizo wa kutaka seva za tume hiyo kuwekwa wazi kwao.

Kamishna huyo alitoroka ambapo akiwa uhamishoni amekuwa akitoa ufichuzi kuhusu mambo yaliyotokea katika tume ya IEBC wakati wakihudumu hapo mwaka 2017.

Mpaka sasa, Akombe anaishi Addis Ababa, jiji ambalo analiita kama nyumbani kwao. Alipakia picha hiyo akifurahi kurudi ‘nyumbani’ baada ya kutembelea mataifa ya Afrika Kusini na Magharibi mwa Afrika.

“Nahisi vizuri kurejea nyumbani #Addis baada ya wiki chache huko Magharibi na Kusini mwa Afrika,” Roselyne Akombe aliandika kwenye Twitter.

Watu mbali mbali walifurika hapo na kumsifia kwa uvaaji mzuri na sura iliyosheheni tabasamu la karne, Miguna Miguna hakuachwa nyuma naye alihakikisha ametilia hongera zake kwa muonekano wa Akombe.

“Unaonekana vizuri daktari, cheers,” wakili Miguna Miguna aliandika.

Akombe alimjibu kwa bashasha huku akimwambia kwamba Wakenya wengi wanamsubiria kwa hamu na ghamu nchini Kenya mwishoni mwa mwezi ujao.

“Asante, Daktari. Timu ya mapema tayari iko karibu kukukaribisha nyumbani mwezi ujao,” Akombe aliandika.

Miguna Miguna siku mbili zilizopita alidhibitisha kuwa rais William Ruto amemkabidhi pasipoti mpya na atarejea nchini tarehe 20 Octoba baada ya zaidi ya miaka 4 akiwa uhamishoni Canada.

View Comments