In Summary

• Wikendi iliyopita Rachier alijitokeza na kusema amekuwa mwanachama katika kundi la Freemason kwa miaka 28.

Mbunge Otiende Amollo amejitenga na madai ya Rachier kuhusu Freemason
Image: Facebook

Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo amejitenga vikali na madai ya uwezekano wake kuwa mwanachama wa kundi lilanochukuliwa kuwa la kishetani – Freemason.

Ilimbidi Amollo kutoa matamshi yake siku moja tu baada ya wakili mwenza katika kampuni yake ya uanasheria, Ambrose Rachier kufichua kwa mapana katika mahojiano na runinga ya NTV kuwa ni mwanachama wa kundi hilo kwa miaka 28 iliyopita.

Wikendi, wakili Rachier ambaye pia ni mwenyekiti wa muda mrefu wa klabu ya soka ya Gor Mahia alifunguka kuwa ni mwanachama wa Freemason na hata kuelezea jinsi mtu anajiunga na pia kuzungumzia uvumi unaozunguka suala zima la kundi hilo linalohusishwa na ushirikina wa kishetani na wengi.

Otiende Amollo ambaye ni mshirika wa karibu wa Rachier katik kampuni yao ya kisheria amejitenga mbali na uwezekano wake pia kuwa mmoja wa kundi hilo.

Kupitia ukurasa wake wa Tweeter, Amollo alionekana kuchekeshwa na hatua ya Rachier kusema yeye ni mwanachama wa kundi hilo na kuweka msimamo wake kuwa hajawahi na kamwe hawezi kuwa mwanachama wa kundi hilo la kishetani.

“Nyakati za Kuvutia! Nimeona Mahojiano na Mshirika Wangu wa Kampuni ya Uanasheria Ambrose Rachier Kuhusu Freemason! Mimi Sipo na Sitajiunga na Freemason! Ifahamike Kwamba Kampuni ya Sheria ya Rachier & Amollo LLP Haihusishwi na Harakati hizo za Freemason,” Amollo aliandika.

View Comments