In Summary
  • Kulingana na Ezekiel wakati wa kulipa mahari hakutoa pesa zozote,bali mke wake alimlipia kiasi cha pesa ambacho kilidaiwa kulipwa
Image: THE STAR
Pete
Image: SERENDIPITY DIAMONDS

Ulipaji mahari ni mjadala ambao umezua hisia mbalimbali na ni utamaduni wa tangu jadi katika jamii za kiafrika .Hata hivyo visa ni vingi tu kuwahusu watu ambao walionekana kuonewa kuhusu kiasi cha mahari iliyoitishwa na jamaa za wenzao wa kike.

Kwa wakati auakarne hii ya sasa iwapo unataka kuishi na mwanamke lazima ulipe mahari.

Vijana wengi wanakwepa majukumu haya kwani, wanahitajika kutumia pesa nyingi ili kumlipia mweni wake mahari,ilhali hana uwezi huo.

Ni wachache ambao huwapata wanawake ambao wamo tayari, kusaidiana katika kulipa mahari.

Nikiwa kwenye ziara zangu nilipatana na Ezekiel(sio jina lake)ambaye alinisimulia kwa nini anampenda mke wake kupita kiasi.

Kulingana na Ezekiel wakati wa kulipa mahari hakutoa pesa zozote,bali mke wake alimlipia kiasi cha pesa ambacho kilidaiwa kulipwa.

"Mke wangu alinilipia mahari, licha ya hayo sijaolewa kama vile wengi hudhani, mwanamke akilipa mahari amemuoa mwanamume huyo

Sikuwa na kazi ambayo ingenifanya nimlipia mke wangu mahari, bali tulikubaliana na akaniambia nisisumbuke kwani atalipa mahari mwenyewe na iiwe siri kati yangu naye

Hata baada ya kunilipia mahari amekuwa amenipa heshima kama mume wake na wala sijawahi ona chembechembe za madharau."

Aliogeza;

"Wakati wa sasa wanandoa wengi hawadumu kwenye ndoa kutokana na kutojuana vyema na kupeana heshima katika ndoa

Mimi na mke wangu tumekuwa kwa ndoa kwa miaka 18, na yote tunamshukuru Mungu, licha ya changamoto za ndoa bado upendo wetu ni kama ndio tumeanza mapenzi yetu, kitu cha muhimu katika ndoa ni kuaminiana na kupeana heshima."

 

 

 

 

View Comments