In Summary
  • Kiongozi huyo aliyeapishwa hivi karibuni alimshukuru Ruto kwa kumteua kushika wadhifa huo, akieleza kuwa ni heshima “aliyoipokea kwa unyenyekevu na shukrani nyingi”.
Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi wakati wa maombi katika ibada ya Jumapili huko Kayole mnamo Agosti 7, 2022.
Image: DPPS

Waziri Mkuu Musalia Mudavadi amemhakikishia Rais William Ruto na Wakenya kwa jumla kuhusu kujitolea kwake kuhudumu kwa bidii.

Kiongozi huyo aliyeapishwa hivi karibuni alimshukuru Ruto kwa kumteua kushika wadhifa huo, akieleza kuwa ni heshima “aliyoipokea kwa unyenyekevu na shukrani nyingi”.

“Ninamuahidi Rais na watu wa Kenya kwamba nitawatumikia kwa kujitolea kabisa kwa uwezo wangu wote na ndani ya mipaka ya Katiba ya Kenya,” alisema Alhamisi.

Alidokeza kuwa anafahamu viongozi hao walikabiliwa na siku ngumu mbeleni katika azma ya kubadilisha hali ya uchumi wa nchi.

Akizungumza baada ya zoezi la kuapishwa katika Ikulu, Ruto alionya baraza la mawaziri kuhusu kibarua kinachowasubiri.

"Niko macho kwa changamoto nyingi ambazo ziko mbele yetu hata tunapoanza kazi ya kubadilisha uchumi wa nchi uliodorora na kurejesha heshima kwa maisha ya watu."

 

 

 

View Comments