In Summary

• DCI waliripoti kuwa majambazi walivamia kituo cha polisi huko Homabay na kuiba bunduki na risasi.

• Bado hawajapata bunduki zingine zilizoibwa.

Image: DCI Kenya Twitter

Mwanaume mmoja amekamatwa na bunduki aina ya G3 inayoaminika kuibwa kutoka kituo cha polisi cha Homabay kupatikana.

Kituo hicho kilivamia siku ya Jumatano, Novemba 16 na silaha kuibwa.

DCI wameripoti kuwa mshukiwa Charles Nyumba Ongany mwenye umri wa miaka 27 alipatikana na bunduki moja aina ya G-3 iliyokuwa na risasi 20 baada ya oparesheni ya kisiri kufanywa na wakaazi wa Homabay.

Maafisa walipata uvumi kuwa silaha hizo zilikuwa zimezikwa kwenye boma la baba yake Charles, jambo lililowasaidia kupata silaha hiyo.

Walivamia boma hilo katika kijiji cha Abuje, Nyando kaunti ya Kisumu na kuchimba sehemu za boma hilo.

"Oparesheni hiyo ilifanywa asubuhi, babake mshukiwa pia anaaminika kuwa miongoni mwa genge hilo hatari. Hata hivyo,  alifanikiwa kutoroka na polisi wanamtafuta," DCI waliandika.

DCI walisema kuwa wana matumaini ya kuwakamata washukiwa wengine baada ya kumkamata Charles kwani atawafichua wenzake na kurejesha silaha zingine.

Waliripoti kuwa majambazi hao walivaamia kituo hicho na kuiba silaha zikiwemo bunduki tatu za G-3, bunduki moja aina ya AK-47 na risasi 110.

Maafisa wa polisi wamezidi kujikakamua kudhibiti usalama nchini Kenya kwa kuimarisha doria ya vikosi maalum na polisi wa kawaida kufuatia kuongezeka kwa visa ujambazi.

Siku ya Alhamisi, Novemba 17, Rais William Ruto aliwapa ruhusa maafisa kutumia silaha zao iwapo majambazi wataleta utata au kujaribu kutoroka.

 

 

View Comments