In Summary

• Nawaalika ili tufanye kazi pamoja. Baadhi ya vita wanavyotaka kushiriki havitawasaidia watu wa Meru - Mwangaza.

Gavana wa Meru akiombewa
Image: Facebook

Baada ya kupata afueni mahakamani, gavana wa Meru Kawira Mwangaza hatimaye amemeza kiburi na kuomba radhi kwa MCAs wa kaunti hiyo ili wasimng’atue madarakani.

Mapema wiki jana, jaji Thripsisa Cherere alisitiza mchakato wa madiwani kuandaa vikao vya kujadili kung’atuliwa kwake kama gavana katika kile alisema kwamba mchakato wenyewe ulikuwa umekiuka vipengele vingi.

Baada ya uamuzi huo wa mahakama ya juu, gavana Mwangaza alijawa na furaha na kuenda kanisani ambapo aliombea na mchungaji na kisha kusema ‘samahani’ mara 70 kwa MCAs hao.

Katika hotuba yake baada ya maombi hayo yaliyoongozwa na mchungaji kukariri ‘Samahani’ hadi mara 70, gavana Mwangaza alisema kuwa madiwani hao walimtaka kuomba msamaha naye akakubali.

Licha ya kukariri msamaha mara 70, gavana alisisitiza kuwa alikuwa anajua fika kuwa hakuwa na makossa hata kidogo lakini kwa sababu tu MCA walitaka msamaha basi hakuwa na budi.

“MCAs walikuwa wamesema, gavana aseme samahani kwao. Hata kama hakuna makosa nimewafanyia. Kwa sababu hawa ni MCAs 69, pamoja na spika jumla wanakuwa 70, nataka tuinue mikono tuwaambie samahani mara 70,” Mwangaza alisema kabla ya mchungaji kuongoza kukariri huko kwa samahani.

Gavana pia alisema milango yake iko wazi kwa MCAs ambao walitaka kufanya kazi naye.

“Nawaalika ili tufanye kazi pamoja. Baadhi ya vita wanavyotaka kushiriki havitawasaidia watu wa Meru. Hata kama nimeshinda mahakamani leo, naomba kwa unyenyekevu waje tujadiliane. Iwapo kuomba samahani kutamaliza matatizo yanayotukabili, naomba msamaha kwa kila mjumbe wa bunge la kaunti,” Bi Mwangaza alisema.

Hoja ya kumtumua madarakati gavana kwa mara ya kwanza iliwasilishwa rasmi katika bunge la kaunti mnamo Novemba 22. MCAs 68 walitia saini ombi hilo huku mmoja akitoroka.

View Comments