In Summary

• Alipuuzilia mbali madai ya Ole Kanchory kuwa watu watatu ndio walifanya Odinga kupoteza uchaguzi.

• Ole Kanchory alikuwa amewataja Junet, Mucheru na Makau Mutua kama waliochangia kufeli kwa Odinga.

Odinga na Kenyatta
Image: Maktaba

Mchanganuzi wa masuala ya Kisiasa, Mutahi Ngunyi amejirusha mazima katika gumzo linalozidi kutokota nchini kuhusu ni kwa nini kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga alipoteza uchaguzi wa Agosti 9.

Gumzo hilo lilianzishawa upya kufuatia Makala ya runinga ya NTV yaliyofanya udhubutu wa kufafanua kwa kina jinsi gani Odinga alibwagwa na Ruto licha ya kuwa na ufuasi mkubwa na uungwaji mkono wa vyama tanzu vingi chini ya mwavuli wa Azimio.

Ngunyi kwa maoni yake kuhusu swali hilo, alitofautiana na aliyekuwa ajenti mkuu wa Odinga, wakili Saitabao Ole Kanchory aliyesema Junet Mohammed, Joe Mucheru na Makau Mutua ndi walikuwa chanzo kikubwa cha Odinga kufeli.

Ngunyi alisema kwa maoni yake aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta ndiye alichangia pakubwa kwa Odinga kupoteza uchaguzi, katika kile alikitaja kuwa ilikuwa ni mbinu fiche ya kutengeneza urafiki naye kwa upande mmoja, na upande wa pili alikuwa anampigia naibu wake William Ruto kampeni za kulinda ahadi yao ya ‘Zangu kumi, zako kumi’

“Kwa mara ya mwisho, Uhuru alitaka KUMkabidhi Ruto. Na hiyo ndio sababu ya Raila Odinga kupoteza uchaguzi. Alifanya AMANI na NAsaba ya Odinga na kutimiza AHADI ya Kumi-Kumi. ALISHINDA kwa pande MBILI,” Ngunyi aliandika Twitter.

Alipuuzilia mbali wale waliozungumza katika Makala ya NTV na kusema kuwa wao waligusia tu vyanzo vya juu juu lakini chanzo halisi na ambacho hawakukitaja ni rais mstaafu Kenyatta.

“Wale wanaozungumza VICHWA kwenye NTV walikuwa kwenye kando tu ya mkakati mzima. Hawa si lolote ila ni wajinga WA KISIASA,” Ngunyi alieleza.

View Comments