In Summary
  • Sonko pia alikuwa anakabiliwa na hadi mashtaka 30 ya utakatishaji fedha, kupokea hongo na mgongano wa maslahi

Sonko aliachiliwa katika kesi ya ufisadi ya Sh20 milioni na hakimu wa kupambana na ufisadi Douglas Ogoti.

Alikuwa ameshtakiwa kwa njama ya kutekeleza kosa la ufisadi yaani ubadhirifu wa pesa za umma za Sh24 milioni kutoka kwa serikali ya kaunti ya Nairobi.

Sonko pia alikuwa anakabiliwa na hadi mashtaka 30 ya utakatishaji fedha, kupokea hongo na mgongano wa maslahi.

Sonko alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Desemba 2019.

Haji alimshutumu Sonko na washirika wake kwa ufujaji wa Sh357 milioni kutoka kwa Jumba la Jiji.

Katika uamuzi ambao ulitolewa na Hakimu Mkuu Douglas Ogoti mnamo Jumatano, Desemba 21, mahakama ilibaini kuwa mashtaka hayangeweza kuthibitishwa bila shaka yoyote.

“Nimeona kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kesi bila shaka yoyote. Kesi nzima dhidi ya washtakiwa wote inaanguka chini ya kifungu cha 210 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPC); sasa wote wameachiliwa,” Ogoti alibainisha.

Sonko na mshukiwa mwenza mfanyabiashara Antony Ombok Jamal walishtakiwa kwa njama ya kuilaghai serikali ya kaunti ya Nairobi takriban Ksh20 milioni mwaka wa 2019.

Huku Sonko akizunguma baada ya uamuzi wa jaji alisema kwamba ameona Mungu akitenda.

"Wacheni Mungu aitwe Mungu. Leo nimeendelea kuona Mkono wake Bwana after being acquited by the anti-corruption court Chief magistrate Hon. Douglas Ogoti. Asante Mungu,"Alisema Sonko.

 

 

View Comments