In Summary

• Wambua alimtaka odinga kutokuwa na nia ya kuwania urais tena ili kumpa Kalonzo nafasi ya kumenyana na Ruto uchaguzi wa urais 2027.

Image: EZEKIEL AMING'A

Uongozi wa chama cha Wiper umeanza mwaka wa 2023 kwa shinikizo kali katika muungano wa Azimio la Umoja One Kenya kwa kutaka vinara wake kumtangaza Kalonzo Musyoka kama mpeperusha bendera wa muungano huo katika uchaguzi wa urais mwaka 2027.

Seneta wa Kituo, Enock Wambua ambaye ni mwandani wa karibu wa Musyoka akizungumza katika mahojiano na runinga ya NTV, alisema kuwa ni wakati sasa kwa Odinga kukubali kuwa muda wake umekwisha na kutofanya jaribio la kuwania 2027 na badala yake kumpa kijiti hicho Musyoka.

“Ninaamini kwamba Raila Amollo Odinga, mtu tunayemheshimu sana na ngome ya ODM ya Nyanza na ngome nyingine za ODM. Wamenufaika kutokana na kujitolea kwa mheshimiwa Stephen Kalonzo Musyoka. Ni sawa tu kwamba wairejeshe ishara hiyo kuanzia Januari hii,” Wambua alisema.

Wambua alisema kuwa muungano huo unafaa kuweka mambo wazi kwa kumtambua Musyoka kama kiongozi wao mapema ili kuanza kumtangaza kote nchini mapema kama ambavyo Ruto alianza kampeni zake miaka kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti mwaka jana.

“Ni lazima tuwe wazi kabisa na mgombea wetu wa urais 2027 itakuwa hivyo ili tupate muda wa kutosha wa kumtangaza mgombea wetu, kuzuru maeneo mengi ya nchi hii iwezekanavyo na kuhakikisha kwamba Wakenya sasa wanaanza kujifahamisha na uwezekano wa urais wa Kalonzo. Ili hilo litokee, lazima tufanye alichofanya Ruto. Ni lazima tuanze kampeni zetu mapema kama jana,” alisema.

View Comments