In Summary

• Charlene aligonga vichwa vya habari baada ya matamshi kuhusu kuwa na ofisi ya binti wa kwanza wa taifa.

Rais Ruto amtetea bintiye Charlene Ruto
Image: Facebook

Rais William Ruto amesimama kidete na kumtetea binti yake Charlene Ruto kuhusu matamshi yake kuwa alikuwa na ofisi ya binti wa kwanza wa taifa.

Akijibu swali la mwanahabari wa runinga ya NTV aliyetaka kujua usemi wake kuhusu matamshi hayo ya binti wake yaliyozua rabsha kwenye mitandao ya kijamii, rais Ruto alifoka vikali akiwataka wale wote wanaomshambulia binti yake kumkoma na kukomaa.

Mwishoni mwa mwaka jana, Charlene alishambuliwa vikali kwa kusema kuwa alikuwa na ofisi ya binti wa kwanza wa taifa, jambo ambalo wengi walielewa kuwa ofisi hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa ushuru wa walipa kodi.

Baadae Charlene alijitokeza na kukana madai hayo huku akisema kuwa ofisi yake ilikuwa ikiendeshwa na fedha zake mwenyewe wala si za walipa ushuru.

Rais Ruto alisisitiza kuwa wanaomzomea bintiye wanafaa kumuelewakuwa ni mtoto na pia kusema kila mtu anajua hakuna ofisi kama hiyo kwa hivyo Wakenya wasikuwe watu wa kulivalia njuga suala dogo kama hilo.

“Mwache binti yangu Charlene peke yake. Kwa hivyo hawa ni watoto, unajua. Wao ni kuwa watoto tu. Sawa. Unajua vizuri, kwamba hakuna ofisi kama hiyo. Unajua huyu ni msichana ambaye ni kuwa yeye mwenyewe, mtoto. Ana nafasi hii na wenzake, unajua. Wenzake wanamsukuma labda tungeweza kufanya hivi, tungeweza kufanya hivi. Lakini unajua, yuko sawa, unajua, yeye ni bintiye William Ruto tu na wakati mwingine hajui kuamua ikiwa rais anatamani na baba,” Rais Ruto alijibu.

Mwishoni mwa mwaka jana, Charlene alifanya ziara kadhaa katika sehemu mbali mbali kote nchini jambo ambalo lilizua maoni kiznani wengine wakisema alikuwa anatumia gharama za walipa kodi kuendeleza mambo yake.

 

View Comments