Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa amewashauri wanaume kujua thamani yao na wasishushwe tamaa kwa kufedheheshwa.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, wanaume hawapaswi kujiona hawana maana kila wanapokosa pesa
Alisema kuwa mtu anapaswa kuzingatia malengo yake ya maisha na kuweka mpango jinsi ya kuyafikia.
Mbunge huyo aliongeza kuwa wanaume wanapaswa kuzingatia ukuaji wao badala ya kukidhi mahitaji ya washirika wengine.
Mheshimiwa Barasa alisema hivyo na kuongeza kwamba hakuna mwanamume anayedaiwa maisha ya kifahari.
"Wanaume, mnapaswa kuacha kujiona hufai bila pesa, nyie hamdaiwi mtu yeyote maisha laini/ya kifahari. Zingatia malengo na ukuaji wako kama mtu."
Haya yanajiri wakati ambapo vijana wengi wako chini ya shinikizo la kupata mali ili kukidhi matakwa ya jamii.