In Summary

• Khan alifariki kufuatia kutokwa damu kwa wingi baada ya kudaiwa kushambuliwa na mpenzi wake Wahome ndani ya makazi yao jijini Nairobi.

• Awali Maxine alikuwa ameachiliwa kwa dhamana baada ya kushtakiwa kwa kumjeruhi Khan.

DEREVA WA SAFARI RALLY MAXINE WAHOME AKIWA ATIKA MAHAKAMA YA MILIMANI
Image: DOUGLAS OKIDDY

Dereva wa magari ya mbio za langalanga Maxine Wahome sasa anachunguzwa upya na huenda akakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake Asad Khan aliyefariki mwishoni mwa mwaka jana kufuatia mzozo wa vita vya kinyumbani.

Awali baada ya mzozo wao uliopelekea Khan kulazwa hospitalini kwa majeraha makali, Wahome alifikishwa katika mahakama na kustakiwa kwa kosa la kumjeruhi mpenzi wake na baadae kuajiliwa kwa dhamana.

Siku chache baadae, mpenzi huyo wake alifariki na sasa mahakama imearifiwa kuwa huenda mashtaka hayo yakabadilishwa na kuwa ya mauaji uchunguzi utakapomalizika.

"Mazingira katika uchunguzi huu yamebadilika kufuatia kifo cha Asad Desemba mwaka jana. Maxine sasa anachunguzwa kwa mauaji na madhara makubwa. Naomba mahakama kutupa muda wa siku 14 zaidi ili tumalize uchunguzi wetu,” Mwendesha mashtaka wa serikali, James Gachoka aliambia mahakama ya Milimani.

Mwendesha mashtaka huyo alisema muda unahitajika ili kukamilisha uchunguzi wote ikiwemo kupokea ripoti ya uchunguzi kutoka kwa sehemu ya tukio ambayo ni nyumba walimokuwa wakiiishi wapenzi hao wawili pamoja pia na kupata ripoti ya DNA kutoka kwa maabara ya serikali.

Hakimu aliamuru kesi hiyo itajwe Januari 30, 2023 kwa maelekezo zaidi. Pia alimwagiza Bi Wahome aendelee kuripoti kwa afisa wa uchunguzi kila Alhamisi.

Bw Khan alikufa hospitalini siku chache baada ya kushambuliwa vibaya mnamo Desemba 12, 2022 katika makazi yake ya Kileleshwa.

Baada ya tukio hilo, alilazwa katika Hospitali ya Nairobi na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Avenue ambako alifariki dunia Desemba 18, 2023.

View Comments