In Summary

• Mwalimu huyo alitoweka Desemba 22 baada ya kumalizika kwa mitihani ya KCSE.

• Hakuna jirani yake hata mmoja aliyegundua kuwa hayupo hadi familia yake ilipokuja kumtafuta Januari 7, 2022.

Mwili wa mwanamke wapatikana umegongelewa misumari
Image: Maktaba

Mwili wa mwanamume mmoja mwalimu aliyetoweka siku kadhaa zilizopita umepatikana ukiwa umewekwa kwenye jeneza na kugongelewa misumari ndani ya nyumba yake katika kaunti ya Nyeri.

Kulingana na taarifa hizo zilizoripotiwa na jarida moja la humu nchini, Joseph Gathong’o mwenye umri wa miaka 40 kutoka kijiji cha Muhoya alikuwa mwalimu wa somo ya kompyuta katika shule ya upili ya Muhoya na alitoweka wiki tatu zilizopita.

Baada ya sakasaka kwa muda huo wote, wakaazi walipigwa na butwaa waliporauka asubuhi ya Alhamisi na kuupata mwili wake umewekwa ndani ya jeneza lililokuwa na muonekano wa boti, mwili wake ukiwa umegongelewa misumari ndani ya ‘boti’ hilo.

“’Mashua", ambayo ilifanya kazi kama jeneza, ilitengenezwa kwa zege zilizofunikwa na kadibodi. Karibu na ‘mashua’, kulikuwa na maua na paraphilia ikiwa ni pamoja na bendera nyeusi, pembe ya ng’ombe na hati-kunjo zilizoandikwa kwa lugha ya kigeni,” Nation waliripoti.

Mwalimu Githong’o alitoweka siku ya Desemba 22 baada ya kumaliza shughuli ya kusimamia mtihani wa KCSE na baada ya kuingia katika nyumba yake, hakuweza tena kuonekana hadharani mpaka mwili wake ulipokuja kupatikana umesulubishwa ndani ya ‘boti’

Hakuna jirani yake hata mmoja aliyegundua kuwa hayupo hadi familia yake ilipokuja kumtafuta Januari 7, 2022.

 

Kulingana na Bi Wanjiru, familia ya mwalimu huyo iliwasilisha ripoti ya kutoweka kwa polisi.

 

Bw William Gitau, mlezi wa boma ambalo marehemu aliishi kwa miaka 14 alisema kuwa alionekana mara ya mwisho mnamo Desemba 19, mwaka jana.

View Comments