In Summary

• Atwoli katika waraka wa COTU kwa rais alisema makampuni hayo yanafaa kushrutishwa kutilia maanani maslahi ya wafanyikazi wao.

Katibu wa COTU Francis Atwoli akutana na rais William Ruto.
Image: HISANI

Katibu mkuu wa chama cha wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli ameitaka serikali kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya makampuni binafsi ya ulinzi ambayo yanawalipa wafanyikazi wao malipo duni.

Katibu huyo alipakia waraka mrefu ambao wameandikia rais Ruto wakimtaka kuchukua hatua na kushrutisha makamouni ya binafsi ya usalama kuboresha mazingira ya kazi kwa walinzi wa kutwa na kucha.

“COTU (K) imepokea idadi ya kutisha ya malalamiko kutoka kwa wafanyikazi wa sasa na wa zamani wa kampuni nyingi za usalama za kibinafsi ambazo zimekataa waziwazi kufuata miongozo ya kima cha chini cha mishahara, licha ya kutangazwa na serikali ya Kenya kuhusu kima cha chini cha mshahara,” sehemu ya waraka huo ilisoma.

COTU ilisema imejaribu kuwafikia wasimamizi wa makampuni hayo ikiwataka wachukua hatua madhubuti za kuafikiana na vigezo vya makampuni ya kibinafsi bila mafanikio.

Walituhumu makampuni hayo zaidi ya 180 kwa kuendeleza unyanyasaji dhidi ya wafanyikazi huku wakimtaka Ruto kuanzisha msako wa kufunga makampuni ambayo hayatafuata sheria za uajiri nchini.

“COTU ingependa kusihi serikali ya rais Ruto kuchukua hatua kali za msako dhidi ya makampuni haya na kuhakikisha kuwa si tu wanapewa kibali cha kuhududmu ili serikali kupata tozo kutoka kwao bali pia kuhakikisha wafanyikazi wao wanapata mshahara mzuri ambao uko juu ya viwango vilivyowekwa,” barua hiyo ilitoa wito.

View Comments