In Summary

• "Nilipata fursa ya kushiriki kifungua kinywa na wapiga kura wangu na watoto wetu kabla ya kufungua tena shule zao" - Muratha.

Mbunge wa Kiambu awapa watu mikate
Image: Facebook

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kiambu Anne Muratha kwa mara nyingine tena amejipata katika gumzo kali mitandaoni baada ya kuonekana kweney picha akigawa mikate na unga kwa baadhi wa wakaazi wa kaunti hiyo.

Itakumbukwa mbunge huyo wa kaunti miezi kadhaa iliyopita pia akiwa kwenye kampeni alijizolea kashfa kali alipoonekana kweney video akiwarushia watu keki kama kuku.

Katika tukio hilo, alishtumiwa vibaya katika kile ambacho wengi walihisi ni dharau kwa watu, jambo lililomsukuma hadi kwa kona na kumfanya kuomba radhi.

Safari hii alifanya heshima kidogo ambapo alionekana aemwapangisha watu foleni ndefu akiwa anawakabidhi mikate na pakiti za unga katika eneo la Ruiru.

“Mapema leo asubuhi nilifanya ziara ya papo kwa papo kwa wananchi wa Wataalam katika eneobunge la Ruiru, kata ya Biashara. Nilipata fursa ya kushiriki kifungua kinywa na wapiga kura wangu na watoto wetu kabla ya kufungua tena shule zao. Hatua zimewekwa ili kuwawezesha vijana wetu (ambao ndio lengo langu kuu) tunapowapa usaidizi ambao wanahitaji kuwa na mafanikio, kuwajibika, na kushiriki katika jamii. Pamoja tutasonga mbele,” Muratha aliandika kwenye rundo hilo la picha.

Baadhi ya wafuasi wake walimpongeza kwa kufanikishia wapiga kura wake utaalamu wa kinywani huku wengine wakimsuta kwa kujitafutia umaarufu kwa kuwapa watu pakiti moja tu ya unga.

“Badala ya kuwapa wakenya wachache unga mmoja kwa mlo mmoja mbona usiishinikize serikali uliyonayo ipunguze gharama ya bidhaa za msingi na sisi sote tutafurahia,” Joseph Kinuthia alimwambia.

“Usimpe maskini samaki tu, mpe nyavu na umfundishe kuvua samaki. Lakini takrima ni dau la uhakika kwa wanasiasa .... maskini hao wataendelea kurudi na vikapu vitupu.....ili kulishwa,” Lucy Wathika alisema.

“Umebarikiwa mkono unaowapa wahitaji. Pia tunahitaji kushughulikia masuala yanayoathiri uzalishaji. Kama vile: Kupungua kwa rutuba ya udongo, mbinu duni za kilimo, uwekezaji katika teknolojia zinazofaa (k.m. uhifadhi na usimamizi wa kuvuna maji, umwagiliaji kwa njia ya matone, uboreshaji wa mnyororo wa thamani na nyingi. zaidi).Sote tuzingatie viwango vya juu vya huduma bora (soma uadilifu,uwazi na uwajibikaji, ubarikiwe,” Francis Ikiugu alimshukuru.

View Comments