In Summary

• "Usiangalie kibanzi kwenye jicho la ndugu yako huku ukipuuza boriti iliyoko kwenye jicho lako mwenyewe!” Olekina alisema.

Olekina akubali Ruto ni rais
Image: Twiter

Seneta wa Narok Ledama Ole Kina ametupa bomu kwa rais William Ruto akimtaka kudhibitisha kwanza iwapo amelipa kodi ya umeme na maji katika maboma yake kote nchini kabla ya kuanza kudai kuwa kila mtu lazima alipe ushuru.

Haya yanakuja siku moja baada ya baadhi ya wandani wa rais Ruto kudai kwamba familia za rais wastaafu Daniel Moi na Uhuru Kenyatta zinafaa kufanyiwa uchunguzi iwapo wanalipa kodi.

Wandani hoa wakiongozwa na seneta wa Nandi Samson Cherargei wanadai kwamba Uhuru Kenyatta ndiye anadhamini mikutano ya kisiasa ya Raila Odinga ambayo imeanza wiki mbili zilizopita akisema hatambui uongozi wa Ruto.

Mikutano hiyo ya Odinga pia imenuia kutoa wito kwa wafuasi wake kususia kulipa ushuru, jambo ambalo wandani wa Ruto wanasema litalemaza mipango ya serikali ya Kenya Kwanza na hivyo kutaka Kenyatta ambaye kulingana nao ndiye mdhamini mkubwa wa mikutano hiyo kufanyiwa uchunguzi iwapo analipa ushuru.

Ledama alimwambia rais Ruto kuwa kielelezo kuonyesha dhibitisho iwapo huwa analipa kodi kwa biashara zake zote kabla ya kuanza kuwatupia wengine maneno kuhusu ushuru.

“Habari za asubuhi nyote? Tunajulikana sana katika kuwafundisha wengine kile wanachopaswa au wasichopaswa kufanya! @WilliamsRuto umelipa bili zako za umeme na maji katika nyumba na biashara zako zote? Usiangalie kibanzi kwenye jicho la ndugu yako huku ukipuuza boriti iliyoko kwenye jicho lako mwenyewe!” Olekina alisema.

View Comments