logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanamitandao wamchana Tundu Lissu baada ya kudai alipata afueni baada ya kifo cha Magufuli

Kwa mujibu wake, Magufuli alikuwa kiongozi mbovu aliyewadhulumu viongozi wengine

image
na Radio Jambo

Makala03 February 2023 - 10:31

Muhtasari


  • Alimfananisha Magufuli na Idd Amin na kusema hakuna kati yao anayestahili kusifiwa kutokana na walichokifanya wapinzani wao

Kiongozi wa Upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amesema kuwa yeye pamoja na viongozi wengine wa upinzani walipumua baada ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kufariki dunia.

Lissu ambaye alirejea Tanzania hivi karibuni baada ya miaka kadhaa nchini Ubelgiji alipokuwa akizungumza wakati wa mahojiano ya moja kwa moja na Clouds TV Ijumaa, 03 Februari 2023, ambapo alifichua kuwa ilikuwa ahueni kubwa kwao kwa upinzani wakati Magufuli alipoaga dunia.

Kwa mujibu wake, Magufuli alikuwa kiongozi mbovu aliyewadhulumu viongozi wengine walioipinga serikali yake na uongozi wake, na kuongeza kuwa hawezi kujifanya na kumzungumzia Magufuli kwa nia njema kama viongozi wengine wamekuwa wakifanya.

Alimfananisha Magufuli na Idd Amin na kusema hakuna kati yao anayestahili kusifiwa kutokana na walichokifanya wapinzani wao.

"Kuna watu wanasema marehemu hazungumzwi kwa mabaya, nauliza hivi Idd Amin baada ya kufa anasemwa kwa uzuri upi, Mtu mwovu akifa watu wanapata ahueni, kifo cha Magufuli kilitupa afueni maana alitutesa sana na wanaodhani hakuna afueni ni wale waliokuwa wananufaidika naye," Alisema Tindu.

Wanamitandao walitoa hisia tofauti huku wakimlani Tundu kwa matamshi yake.

rushunjufrido: Una laana siyo Bure we waona mabaya tu hakuna mazuri alifanya chuki zako binafsi hazitakusaidia zaidi ya kuendelea kujishusha thamani Mpuuzi tu mmoja

johnyusuph711: Acha zako wewe, ahueni umepeta wewe na tofauti zenu sisi wengine tulimhitaji.

mustafamulimbo: We teteya ugali wako muze ila muto unakusubiri mbiguni๐Ÿ‘

andrewpius72: Nadhani ni Upumbavu zaidi, kuliko umuhimu wa jambo lenyewe, ukikosa hoja ni bora kutulia kuliko kuacha kutulia na watu wakajua Upumbavu wako. Macho yanaona kama miwani haioni vzr kilichofanyika.

izbet_shija: ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ ahueni ya wasio julikana labda. ila maisha magumu ni pale pale

fficialaine3: Ila huyu licha Mungu kumnusuru na kifo bado anamuongelea vibaya Magufuli ๐Ÿ˜ฎ๐Ÿ˜ฎ๐Ÿ˜ฎ utasema yeye atabaki tena milele! Na akimaliza tena miaka miwili hapa Tanzania nimekaa pale.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoยฉ Radio Jambo 2024. All rights reserved