In Summary
  • "Mradi unaendelea, na mwanakandarasi yuko kazini. Ksh50 milioni za ziada zimepatikana kwa ajili ya kukamilika," Jalang'o alisema.
RAIS WILLIAM RUTO NA MBUNGE WA LANG'ATA FELIX ODUOR
Image: JALANG'O/TWITTER

Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) mnamo Jumanne, Februari 7, kilikagua ripoti za wabunge tisa wanaodaiwa kumtenga kiongozi wa chama, Raila Odinga na kumuunga Rais William Ruto.

Ripoti zilionyesha kuwa wabunge 98wa ODM na mbunge wa kujitegemea walikutana Ikulu, ambapo kimsingi walimwacha kiongozi wa Azimio na kuahidi kufanya kazi na serikali tawala.

Jalang'o alishiriki picha na Rais Ruto katika Ikulu, akithibitisha kuwa alikuwa miongoni mwa wabunge waliopata kifungua kinywa na mkuu wa nchi.

“Nilifuatilia tarehe ya kuanza kwa ujenzi wa nyumba za bei nafuu katika wadi ya Highrise na kukamilika kwa Lang’ata TVET.

"Mradi unaendelea, na mwanakandarasi yuko kazini. Ksh50 milioni za ziada zimepatikana kwa ajili ya kukamilika," Jalang'o alisema.

Ruto kwa upande wake amethibitisha kuwa kiini cha mkutano huo ni kuwezesha ushirikiano kutoka kwa viongozi wote katika azma ya kutatua changamoto za nchi.

"Viongozi lazima washikane mikono, waimarishe kuishi pamoja na kufanya kazi pamoja katika kukabiliana na changamoto zinazokabili nchi/yetu. Lazima wajitahidi kuwa mfano na kutumikia maslahi ya wananchi. Hii ni njia ya uhakika ya Kenya iliyoungana na iliyoendelea.

 

 

 

View Comments