In Summary

• Baadhi walimkashifu Salasya kwa matamshi yake wakisema kuwa kiongozi wa aina yake hakufaa kutoa maneno kama hayo.

Salasya ajipata pabaya kwa kusema atampa Toto mimba
Image: Maktaba

Watu kwenye mitandao ya kijamii wamemkaripia mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salsya kufuatia matamshi yake kuwa anamtunga mwakilishi wa Bomet Linet Toto mimba.

Matamshi hayo ya Salasya yalikuja siku moja baada ya mbunge huyo wa kaunti kunukuliwa akimzomea kinara wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga katika kile alikitaja kama siasa duni za miongo mingi.

Toto wikendi iliyopita katika hafla ya kumkaribisha nyumbani mbunge wa Mogotio Reuben Kiborek alimchamba Odinga akisema kuwa siasa zake zilianza hata kabla yake kuzaliwa na mpaka sasa hivi bado zinaendelea bila kufua dafu.

“Huyu mzee Raila Odinga alianza siasa zake za maandamano hata kabla sijazaliwa. Alianza siasa mwaka 1997 wakati sikuwa nimezaliwa na mpaka sasa bado anasema aliibiwa,” Linet Toto alisema.

Mbunge Salasya katika hotuba yake kwenye mkutano wa Azimuo kaunti ya Busia alimkaripia Toto akisema kuwa kitu anahitaji ni mimba ili kutulia.

“Kuna mwengine alichaguliwa kama hana pesa kama mimi, anaitwa Toto nitaenda kukaweka wiki kesho,” Salasya alisema.

Matamshi hayo ya Salasya hata hivyo hayakupokelewa vizuri na baadhi ya wanamitandao ambao walimsuta na kusema kuwa hivyo ni vitisho vibaya sana ambavyo vinaweza tafsiriwa kama njama ya kutaka kumbaka Toto.

“Aibu kwako Salasya. Nilidhani kuna kipengele kinachoonekana cha kiongozi ndani yako lakini unapaswa kuwa huko nje kuwaburudisha watu. Nenda mos,” Ann Wanjiru alisema.

“Hii inatisha sana kwamba viongozi wetu wa kiume wanaweza kuzungumza kwa njia kama hii kuhusu wanawake katika mwaka wa 2023. Hakuna mtu anawafunza wanasiasa wetu jinsi ya kutoa hotuba zao za hadhara, kuna woga mkubwa wakati anazungumza kuwa mimba, ninahofia sana mheshimiwa Toto. Yeye ni kiongozi na hafai kuzungumza kwa njia hii kwa sababu anatoa mfano mbaya sana kwa viwango tofauti na vingi,” mtangazaji Chito Ndlovu alisema.

 

View Comments