In Summary

•Ufadhili wa Sakaja uliwasilishwa kwa binti huyo na naibu gavana Njoroge Muchiri.

Petronila Muthoni, binti aliyeongoza KCPE eneobunge la Embakasi Kusini.
Image: Twitter

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja na naibu wake Njoroge Muchiri wametoa msaada wa karo ya shule kwa mwanafunzi ambaye familia yake ilipata ugumu wa kumpeleka shule ya sekondari.

Sakaja alipakia video ya naibu wake akimpokeza binti huyo hundi wakiwa na baba yake katika ofisi ya naibu gavana.

Sakaja alisema kuwa binti huyo kwa jina Petronila Muthoni kutoka eneobunge la Embakasi Kusini alipata alama 419 katika mtihani wa mwaka jana wa KCPE na kuibuka kidedea katika eneobunge hilo zima.

Gavana Sakaja alitoa taarifa njema kwamba uongozi wake ulihakikisha umelipa karo ya miaka mine ya sekondari kwa ajili ya masomo ya binti huyo.

“Asante @JNjorogeMuchiri kwa kupitisha usaidizi wetu kwa Petronila Mutono aliyepata alama 419 jna kuwa wa kwanza kwa Embakasi Kusini lakini hakuwa na ada. Tumeweka ada za Petronila kwa miaka yake yote 4 ya Shule ya Upili. Petronila endelea na uwe mzuri! Ulimwengu ni wako,” Sakaja alimtakia kila la kheri binti huyo mdogo.

Msaada wa ufadhili wa masomo kutoka kwa gavana huyo wa Nairobi unakuja wakati ambapo wazazi wengi wanazidi kukuna vichwa kuwaingiza watoto wao katika shule za upili kufuatia ugumu wa maisha na gharama ghali.

Wadadisi wa masuala ya kibiashara wanahoji kuwa ugumu wa maisha nchini umechangiwa pakubwa na kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Kenya dhidi ya dola ya Kimarekani kufuatia kudorora kwa uchumi wa nchi.

Jumapili katika ibada ya madhehebu mbalimbali kaunti ya Nakuru, rais William Ruto alisema kuwa ugumu wa maisha umechangiwa na ukosefu wa mvua kwa muda mrefu ambao umesababisha njaa kwa mamilioni ya Wakenya.

Rais alitoa wito kwa Wakenye kuhudhuria hafla ya maombi ambayo itafanyika katika uwanja wa Nyayo Jumanne Februari 14 sambamba na sherehe za wapendanao – Valentino.

 

View Comments