In Summary

• Letoo amekuwa akipigia debe ndoa za Mume mmoja na wake wengi akisema lengo lake ni kuhakikisha kila mwanamke anapata mume.

Muhoozi azindua harakati za kupinga ndoa ya wanawake wengi.
Image: Facebook, Twitter

Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa rais wa muda mrefu wa Uganda ambaye pia ni mkuu wa majeshi ya nchi kavu ya taifa hilo amepinga vikali takwa la baadhi ya watu kueneza sarakasi na kampeni za ndoa yenye wanawake wengi.

Vile vile, Muhoozi amesisitiza katika ndoa ya kawaida ya mwanamke mmoja na mwanamume mmoja, akipiga chini vikali mjadala wa ndoa na mapenzi ya jinsia moja – mjadala ambao umekuwa ukienea kwa kasi katika taifa la Uganda na Kenya kwa Zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Kainerugaba alisema kwa msisitizo mkubwa kwamba katika harakati zake, wafuasi wake wote wanafaa kujua kwamba sheria ni mwanamke mmoja kwa mwanamume mmoja – chochote kinyume na hilo hakina nafasi wala mjadala, kwani Biblia ndivyo inavyowafunza.

“Katika harakati za Muhoozi Kainerugaba, tunaamini katika ndoa za Mwanaume Mmoja, Mwanamke Mmoja! Ndivyo Kristo anatufundisha!!!” Kainerugaba alisema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Hili linalenga mkuki mkali katika harakati za mwanahabari Stephen Letoo ambaye kwa muda sasa amekuwa akipigia debe ndoa za mitala – ambapo anataka bei ya mahari kupunguzwa ili kumpa kila mwanamume afueni ya kuoa mwanamke Zaidi ya mmoja.

Letoo ambaye alijitangaza kuwa rais wa kongamano la wanaume, na kiongozi wa muungano wa wanaume wenye wake wengi amekuwa akisisitiza umuhimu wa ndoa za aina hiyo, akisema lengo si kupiga vita mke wa kwanza bali ni kusitiri wanawake wengi kwa kuhakikisha kwamba kila mwanamke anapata mke na boma la kuita kwake.

View Comments