logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Ni mweupe kama theluji,'Wakili wake pasta Ezekiel asema

Haya yanajiri baada ya kasisi Ezekiel wa New Life Prayer Centre and Church kukamatwa

image
na Radio Jambo

Habari27 April 2023 - 11:41

Muhtasari


  • Akizungumza siku ya Alhamisi, wakili huyo alisema hajui kama Mchungaji Paul Mackenzie wa Good News International Church ana uhusiano wa karibu na Ezekiel.
Pasta Ezekiel akamatwa, mbunge wa Magarini amtetea vikali.

Wakili wa mwinjilisti Ezekiel Odour, Jared Magolo, amesema polisi hawatapata chochote kuhusu mchungaji huyo.

Akizungumza siku ya Alhamisi, wakili huyo alisema hajui kama Mchungaji Paul Mackenzie wa Good News International Church ana uhusiano wa karibu na Ezekiel.

“Tumezungumza na maafisa hao na wanaendelea na uchunguzi watatujulisha kinachoendelea,” alisema.

Alisema mchungaji huyo atatambuliwa na polisi mara watakapomaliza kumhoji.

Wakili huyo alipoulizwa iwapo anajua alipo mke wa mchungaji Ezekiel, alisema hajui kuwa ana mke.

Haya yanajiri baada ya kasisi Ezekiel wa New Life Prayer Centre and Church kukamatwa Alhamisi asubuhi.

Kasisi huyo, mnamo Jumatano, alihojiwa kwa saa nyingi kwa madai kuwa kanisa lake linajihusisha na uchawi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Rhodah Onyancha alisema kuna madai ya vifo vilivyoripotiwa katika eneo lake.

Polisi walisema hatua ya kumwita Jumatano ilichochewa na uchimbaji wa miili unaoendelea kutoka shambani katika Msitu wa Shakahola.

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved