In Summary

• Atwoli alisema kuwa yeye hawezi kumshauri Odinga kitu chochote kwani ni kama kaka mkubwa aliyeanza siasa akiwa na miaka 14.

FRANCIS ATWOLI
Image: CHARLENE MALWA

Kiongozi wa muungano wa wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli ametoa wito kwa viongozi walio karibu na kinara wa upinzani Raila Odinga pamoja na rais Ruto kuwapatanisha ili kuzuia maandamano ambayo yamepangwa kurejelewa Kesho Jumanne.

Akizungumza katika sherehe za kuadhimisha siku ya wafanyikazi jijini Nairobi, Atwoli hata hivyo alisema kuwa ni wakati sasa kila mtu akiwemo Odinga kukubali na matokeo ya urais ili kupisha ukuaji wa uchumi.

Atwoli alisema kuwa anamjua vizuri rais Ruto pamoja na Odinga ambaye alimtaja kama ndugu yake mkubwa na kusema wote wanaweza kupata mwafaka pasi na kurejelewa kwa maandamano ambayo yatalemaza shughuli za wakenya wa kawaida.

Atwoli alisema yeye hawezi kumshauri Odinga kitu chochote kwa sababu ni ndugu mkubwa aliyeanza siasa akiwa na miaka 14.

“Mimi siwezi kumshauri Raila Odinga kitu chochote kwa sababu alianza siasa akiwa na miaka 14 tu, mimi ni nani wa kumshauri,” Atwoli alisema.

Katibu huyo wa COTU alirejelea matukio ya kisiasa mwaka jana akisema kuwa yeye alikuwa kinara katika kumpigia debe Odinga lakini wakati matokeo yalipotoka, alikuwa mtu wa kwanza kukubali akiwa kwao Magharibi alipowaambia watu kuwa Ruto ameenda na kiti.

Alimtaka Odinga pia kukubali kama yeye na kuungana katika kulifanyia taifa kazi, akitoa pia wito kwa Ruto kumtafutia kazi Odinga serikalini ili kumsitiri kwani kuna watu aliosena anawajua na ambao walitumia jina la Odinga kujinufaisha kibinafsi.

View Comments